Yanga 1-1 Simba, Kelele nyingi, ufundi ‘zero’

NA ERNEST CHENGELELA (OUT) KAMA kawaida pambano la Yanga na Simba lilikuwa lenye tambo nyingi nje ya uwanja, lakini ndani likashindwa kuthibitisha ubora wake kiufundi, mipango na mbinu. Ndani ya dakika 26 za pambano hilo tayari maamuzi na nidhamu mbovu zilishaharibu mchezo huo, ambao uliisimamisha Tanzania kwa dakika 90 kutokana na kelele zake, lakini si ubora wake uwanjani. BINGWA lilikuwepo […]

Kariakoo derby Si kwa ‘undava’ huu

NA MARTIN MAZUGWA, DAKIKA 90 za watani wa jadi zilimalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo uliokuwa na presha kubwa kwa waamuzi wa mchezo huo, Martin Saanya mwamuzi wa kati, Samwel Mpenzu, Ferdinand Chacha na Elly Sasii  kushindwa kumudu na kwenda na kasi ya mchezo huo. Mchezo huo uliotawaliwa na ubabe mwingi kwa wachezaji kuchezeana rafu, kama waamuzi […]

Kichuya afunga… Bao la rekodi duniani

NA HASSAN DAUDI, MOJA kati ya mabao matamu yaliyowahi kutokea katika mchezo wa mahasimu Simba na Yanga ‘Kariakoo derby’ ni lile lililofungwa juzi na staa Shiza Kichuya. Katika mtanange huo ambao timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1, Kichuya ndiye aliyeisawazishia Simba, baada ya Amis Tambwe kuitanguliza Yanga katika dakika ya 26. Kichuya alifunga bao hilo kwa mpira wa kona […]

Namna Chelsea walivyocheka kwenye mfumo mpya wa 5-3-2

LONDON, England BAADA ya kupokea vichapo mfululizo kutoka kwa Liverpool na Arsenal, Kocha Mkuu wa Chelsea, Antonio Conte, aliamua kubadili mfumo wake ndani ya kikosi na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Hull City juzi Jumamosi. Conte alivyokuwa akiinoa Juventus na timu ya taifa ya Italia, alijulikana kwa mapenzi yake ya kutumia mfumo wa mabeki watatu […]

Eti Lahm hajaridhishwa na makali ya Bayern!

MUNICH, Ujerumani BEKI wa pembeni wa Bayern Munich, Philipp Lahm, haamini kuwa wamefikia ubora wanaoutaka wakiwa chini ya kocha Carlo Ancelotti. Kauli ya nyota huyo imekuja ikiwa ni baada ya Bayern kushindwa kuendeleza wimbi lao la ushindi katika ligi kwa kutoa sare ya bao 1-1 na Cologne. Wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani, Allianz Arena, Bayern walikuwa wa kwanza kufunga […]

Kama ulimponda Cavani pole

  LONDON, England STRAIKA Edinson Cavani ameonesha kuwa anaweza kuziba pengo la Zlatan Ibrahimovic pale PSG, baada ya kuendeleza moto wake wa kuwatungua walinda mlango. Katika mchezo wa juzi dhidi ya Bourdeaux, Cavani alipasia nyavu mara mbili na kuiwezesha PSG kuibuka na ushindi wa mabao 2-0. Mpaka sasa, fowadi huyo wa Uruguay ameshapachika mabao 11 katika michezo tisa ya mashindano […]

Mashabiki West Ham watiwa mbaroni

LONDON, England WATU watatu wanaodaiwa kuwa ni mashabiki wa klabu ya West Ham wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani. Mashabiki hao wanatajwa kuwa sehemu ya vurugu zilizotokea juzi katika mchezo kati ya West Ham na Middlesbrough, ambapo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. Polisi walilazimika kuwasindikiza mashabiki wa Middlesbrough baada […]

Guardiola akaribishwa England, Man United yabanwa nyumbani

LONDON, England Tottenham imemuonyesha kwa mara ya kwanza Pep Guardiola uchungu wa kufungwa tangu atue Ligi Kuu England, baada ya kuichapa Manchester City mabao 2-0, huku mahasimu wao, Manchester United, wakitoka sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Old Trafford, dhidi ya Stoke City. Spurs walianza kwa kasi mchezo huo uliochezwa White Hart Lane na kupata bao dakika ya tisa, baada […]

Madrid yapata sare ya nne mfululizo

MADRID, Hispania Real Madrid wameendelea kukumbwa na kutoka sare mechi ya nne mfululizo, safari hii wakibanwa na Eibar na kutoka sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu. Watu wa mji wa Eibar wanaweza wakaingia kwenye uwanja huo wa Bernabeu mara tatu, lakini timu yao imefanikiwa kutingisha nyavu za Madrid katika safari yao hii ya tatu dhidi ya miamba […]

Pluijm awashika uchawi akina Ngoma

NA ZAINAB IDDY, KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, amewashika uchawi wachezaji wake baada ya kusema walizembea kupata ushindi dhidi ya Simba, katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, iliyochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Akizungumza na BINGWA juzi, Pluijm alisema uzembe wao ulitoa mwanya kwa Simba kutawala mpira na kusawazisha bao […]