Kocha wa Azam awapotezea Okwi, Kagere

ZAITUNI KIBWANA KOCHA wa Azam, Meja Mstaafu Abdul Mingange, amesema hatapoteza muda kuwachunga washambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi na Meddie Kagere, kuelekea mchezo wao utakaochezwa Jumatatu ya wiki ijayo. Azam itawakaribisha Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Akizungumzia mchezo huo, Mingange alisema anakiandaa kikosi chake kwa ajili ya kuondoka na […]

Kuiona Sevilla Taifa buku tano

MWANDISHI WETU SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kushirikiana na SportPesa, wametangaza viingilio vya mechi ya kihistoria kati ya mabingwa watetezi Ligi Kuu Bara, Simba dhidi ya Sevilla ya Hispania itakayochezwa Mei 23, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa TFF, Cornel Barnaba, […]

Hawachekani

WINIFRIDA MTOI MIAMBA ya soka nchini Tanzania, Simba ambao ndio vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Yanga wanaoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo, jana wote wamechezea kichapo cha bao 1-0 kila mmoja. Vinara hao wa ligi na mabingwa watetezi Simba, wao jana walikuwa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam kukipiga na wababe wao kwa msimu […]

Uongozi mpya Yanga: Msimu ujao zamu yetu

Hussein Omar SIKU chache baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Yanga, Dk. Mshindo Msolla, amefunguka baadhi ya mipango yake kwa ajili ya klabu hiyo ambayo itamfanya aache alama Jangwani. Mshindo alisema moja ya alama hizo ni pamoja na klabu hiyo kutwaa mataji mengi msimu ujao na kujiendesha yenyewe bila kutegemea fedha za mtu binafsi. “Nafahamu kwamba mashabiki wa Yanga wamekosa […]

Vikosi Simba VS Kagera Sugar vilivyoanza leo

Lulu Ringo, Dar es SalaamTimu ya Simba SC tayari imeshuka katika dimba la Taifa kumenyana na Timu ya Kagera Sugar leo Ijumaa Mei 10 ikiwa ni mechi ya marudiano. Simba inashuka dimbani ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa goli 2-1, dhidi ya Kagera Sugar. Kikosi cha Simba SC; Aishi Manula Zana Coulibaly Mohamed Hussein Erasto Nyoni James Kotei Hassan Dilunga Mzamiru […]

Aunt Ezekiel akana kushindwa kuuza pombe

NA JEREMIA ERNEST MWIGIZAJI nyota Bongo, Aunt Ezekiel, amesema hajashindwa kuendesha biashara yake ya kuuza pombe katika pub yake iliyopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam, bali amepata sehemu nyingine. Akizungumza na Papaso la Burudani, Aunt alisema kufungwa kwa pub hiyo kumefanya baadhi ya watu waseme amefulia, jambo ambalo si la kweli.  “Sijashindwa kuendesha ‘pub’ yangu, ila nimepata eneo ambalo ni […]

Tanasha hana mpango wa kujiunga WCB

NA BRIGHITER MASAKI BAADA ya kuachia ngoma yake ya kwanza inayoitwa Radio, mpenzi wa Diamond Platnumz, Tanasha Donna, ameweka wazi kuwa hana mpango wa kujiunga na lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB). Mrembo huyo kutoka Kenya ambaye pia ni mtangazaji wa redio NRG, ameonyesha nia ya kuendelea kufanya muziki mara baada ya wimbo wake huo kupokewa vizuri na mashabiki wa […]

Timu hizi zilisubiri hadi siku ya mwisho kutwaa taji EPL

LONDON, England BAO murua la nahodha wa Manchester City, Vincent Kompany, lilirudisha matumaini ya timu hiyo kutwaa taji la Ligi Kuu ya England msimu huu. Ulikuwa usiku ambao kocha wa kikosi hicho, Pep Guardiola, alifufua hisia mpya za kuamini kuwa wana uwezo wa kutwaa taji hilo kwa mara ya pili mfululizo, huku ikiwa ni mara ya kwanza kwa Manchester City […]

Spurs, Liverpool wametuletea tena unafiki wa Waingereza 

NA AYOUB HINJO KWA urahisi tu, inaaminika kwa kiasi kikubwa Watanzania hatuna utofauti na Waingereza, hata hivyo labda kwa vitu vichache tu. Kama mchezo wa soka ungekuwa unachezwa midomoni basi England wangekuwa mabingwa katika kila mashindano au michuano iwe ya Ulaya au dunia, wale watu wanaongea hasa. Siku moja, rafiki yangu aliwahi kuniambia kuwa tofauti ya Waingereza na Watanzania ni […]

Bayern wamkataa kocha Ajax

MUNICH, Ujerumani MTENDAJI Mkuu wa Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge, amekanusha kuwa wanamtaka kocha wa Ajax, Erik ten Hag. Awali, zilikuwapo taarifa kuwa Bayern wanataka kuachana na mkuu wa benchi lao la ufundi, Niko Kovac, jambo ambalo Rummenigge amelikanusha. Lopetegui hana kazi tangu alipotimuliwa Real Madrid mwishoni mwa mwaka jana, akiwa ameiongoza timu hiyo katika mechi 14 tu. Sarri akiri maji […]