Kumbe usajili wa Domayo Azam ulitaka kumtoa roho Jemedari 

NA ABDULAH MKEYENGE SIMULIZI ya usajili wa kiungo wa Azam FC, Frank Domayo ‘Chumvi’, kujiunga na timu hiyo mwaka 2014 akitokea Yanga haikuwa nyepesi hata kidogo, ilikuwa ni jasho na damu. Usajili huo uliowakera mashabiki wa Yanga na kumpa wakati mgumu aliyekuwa meneja wa kikosi hicho, Jemedari Said ambaye ndiye aliyecheza sinema nzima ya ‘kininja’ kuhakikisha Domayo anakuwa mchezaji wa […]

Pogba, Sanchez wachafua hali ya hewa Man Utd

LONDON, England MASTAA Paul Pogba na Alexis Sanchez, wanadaiwa kuwa chanzo cha kuzuka mgawanyiko kwenye vyumba vya kubadilishia jezi vya Manchester United, kutokana na kiasi kikubwa cha fedha ambacho wanalipwa wanapofunga bao na kutoa ‘asisiti’. Wawili hao wanadaiwa kuwa na mikataba minono katika klabu hiyo ya  Manchester United na ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa fedha nyingi. Kwa mujibu wa gazeti […]

Van Dijk alamba tuzo nyingine EPL

LONDON, England STAA Virgil van Dijk amesema ni heshima kubwa kutangazwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Ligi Kuu England, baada ya kushinda kura za mashabiki, manahodha wa timu na jopo la wataalamu wa soka. Beki huyo wa kati wa Liverpool mwenye umri wa miaka 27, anakuwa wa kwanza kukabidhiwa tuzo hiyo tangu alipofanya hivyo wa Manchester City, Vincent Kompany, […]

Man City yaweka rekodi, yatetea ubingwa EPL

LONDON, England YAMETIMIA, hivyo ndivyo unavyoweza kuzieleza mbio za Ligi Kuu England zilizokamlika rasmi jana kwa timu ya Manchester City kufanikiwa kutetea ubingwa wake. Kwa kufanikiwa kutwaa taji hilo, Man City wamekuwa timu ya kwanza kutetea ubingwa wake tangu msimu wa 2008-09 wakati Manchester United walipofanikiwa kufanya hivyo na hivyo kuwaacha tena Liverpool wakiondoka kapa kwa mara nyingine tena tangu […]

Wakongwe wamng’ata sikio Msolla

NA HUSSEIN OMAR WACHEZAJI wa zamani wa Yanga wamemtaka Mwenyekiti mpya, Mshindo Msolla, kutorudia makosa yaliyofanyika nyuma na kuchagua watu wasiofaa katika kamati mbalimbali ambazo zitaundwa na Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo. Mmoja wa wakongwe hao ni beki wa kushoto, Anwar Awadh ambaye alimshauri Msolla kuwaweka watu wa mpira na kuachana na wale ambao hawataweza kuisaidia Yanga. “Kama kuna […]

Simba vs Azam FC …AFE PUNDA, MZIGO UFIKE

NA HUSSEIN OMAR AFE punda, mzigo ufike! Ndio msemo rahisi unaoweza kusema pale Simba watakapowavaa Azam FC, huku kila mmoja akihitaji ushindi kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi. Simba na Azam FC leo zitashuka katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, kuumana katika mfululizo wa michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara. Katika msimamo wa ligi, Simba licha […]

Kakolanya aziita mezani Simba, Azam FC

ZAINAB IDDY BAADA ya kuachana rasmi na Yanga, mlinda mlango, Beno Kakolanya, amesema kwa sasa yupo tayari kukipiga katiki timu yoyote inayomhitaji. Kakolanya alikuwa na mgogoro na Yanga kwa zaidi ya miezi sita sasa, huku akiwa amepeleka malalamiko yake Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) akiomba kuvunja mkataba wake. Kakolanya aliliambia BINGWA, anashukuru Mungu suala lake limemalizika hivyo yupo huru kwenda […]