Minziro: Naiandalia Simba dozi ya kushtua

WINFRIDA MTOI KOCHA Mkuu wa Singida United, Fred Minziro, amesema kuna uwezekano wa kukutana na Simba ikiwa imeshatangaza ubingwa, hivyo atawaandalia dozi itakayowashtua. Singida United juzi ilitoka sare ya mabao 2-2 na JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Namfua, Singida, mechi inayofuata watakutana na Simba, Mei 21 katika dimba hilo. Akizungumza na BINGWA jana, Minziro, alisema baada ya kutoka sare ya […]

Ushindi waisahaulisha Coastal kipigo cha 8-1

OSCAR ASSENGA, TANGA KOCHA mkuu wa timu ya Coastal Union, Juma Mgunda, amesema ushindi walioupata wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mechi ya Ligi Kuu soka Tanzania Bara, umewabadilisha fikra za kufungwa mabao 8-1 na Simba. Mgunda aliyasema hayo mwishoni mwa wiki mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo, iliyochezwa kwenye Uwanja wa CCM Mkwakwani mjini Tanga, ambapo […]

Kagera kuwapa wachezaji Simba, Yanga

ZAINAB IDDY KOCHA wa Kagera Sugar, Mecky Mexime, amesema kuwa yupo tayari kuwatoa wachezaji wote watakaohitajika na timu za Simba na Yanga ili aijenge timu upya. Akizungumza na BINGWA, Mexime alisema hana shaka na ubora wa ufundishaji wake, hivyo hata kama wakiondoka wachezaji wote ana uwezo wa kuisuka upya timu yake. “Ni kawaida kwa Simba na Yanga kuchukua wachezaji katika […]

Katwila: Simba jiandaeni tunakuja

ZAITUNI KIBWANA KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zubery Katwila, ametoa mkwara mzito kwa wapinzani wao Simba kuwa wasitarajie mteremko watakapovaana nao keshokutwa. Simba itawakaribisha Mtibwa Sugar Alhamisi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Akizungumza na BINGWA jana wakati akirejea kutoka mkoani Tanga, Katwila alisema licha ya mechi kuwa karibu karibu lakini Simba […]

Amri Said: Pointi tisa tu zinatosha kubaki TPL

ZAITUNI KIBWANA KOCHA Mkuu wa Biashara United, Amri Said, amesema anasaka pointi 12 ikishindikana apate tisa ili kuibakisha timu yake Ligi Kuu Tanzania Bara. Biashara United imebakisha mechi nne pekee kabla ya kumalizika kwa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikishika nafasi ya 18 kati ya mechi 35 ilizocheza, ikikusanya alama 40 pekee. Akizungumza na BINGWA jana, Amri Said, alisema ikishindikana kupata […]

Wadau, wanamuziki wa dansi jiongezeni kwenye hili

CHRISTOPHER MSEKENA KATIKA vilinge mbalimbali vya muziki wa dansi hapa Tanzania si jambo la ajabu sana kukuta mijadala yenye hoja kuhusu uhai na kifo cha muziki huo hasa kipindi hiki ambacho Bongo Fleva imeshika hatamu. Mijadala hiyo inapata nafasi kutokana na ukweli kwamba mambo yanayoongeza hamasa kwa mashabiki kufuatilia dansi yamepungua kwa kiasi kikubwa kwenye vichwa vya habari za burudani […]

Aiyee aitolea nje Simba

ZAINAB IDDY KINARA wa mabao katika kikosi cha Mwadui FC, Salim Aiyee, ameitolea nje Simba baada ya kusema kuwa hawezi kusaini kwa Wekundu wa Msimbazi. Aiyee aliyeifungia Mwadui FC mabao 16 na kuwa kwenye mbio za ufungaji bora msimu huu, ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuhitajika na kocha Mbelgiji, Patrick Aussems. Akizungumza na BINGWA jana, Aiyee alisema licha ya kuwepo […]