Eti Balotelli atarejea England akiwa mpya!

LONDON, England WAKALA wa straika, Mario Balotelli, Mino Raiola, amesema kwamba mteja wake huyo atarejea tena nchini England mwakani akiwa moto wa kuotea mbali. Kauli ya wakala huyo imekuja ikiwa ni baada ya Balotelli kufufua matumaini ya kurudi kwenye ubora wake baada ya kucheza kwa kiwango cha juu katika mechi zake mbili za mwanzo akiwa na klabu yake mpya ya […]

Mashabiki wataka Mourinho afukuzwe

LONDON, England HALI si shwari kwa kocha, Jose Mourinho, hasa baada ya mwenendo unaoonekana kutowaridhisha mashabiki wa klabu ya Manchester United. Kwa lugha nyepesi na ya kueleweka, kocha huyo ameanza kukumbana na presha ya mashabiki ‘wendawazimu’ wa Old Trafford. Baada ya Sir Alex Ferguson kutundika daluga, David Moyes, alikumbana na presha hiyo kama ilivyokuwa kwa Louis van Gaal ambaye kuondoka […]

Kiiza mzigoni tena kesho Sauzi

NA EZEKIEL TENDWA, BAADA ya kuanza mikikimikiki ya ligi kuu nchini Afrika Kusini kwa kucheza mchezo mwishoni mwa wiki iliyopita, straika wa zamani wa Simba, Hamis Kiiza, kesho anatarajiwa kuonyesha tena makeke yake kwenye kikosi chake cha Free State Stars kitakachowakabili Golden Arrow. Kiiza alianza kuitumikia timu yake hiyo wiki iliyopita walipocheza na Bloemfontein Celtic, mchezo ambao ulimalizika kwa suluhu […]

Kilimanjaro Queens kamili kutwaa ndoo leo

Soka ya Wanawake Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens, leo inatarajiwa kuvaana na Kenya katika mchezo wa fainali wa Kombe la Chalenji kwenye Uwanja wa Ufundi uliopo Njeru, mjini Jinja, Uganda. Timu hiyo ya Bara ilitinga fainali baada ya kuwatoa wenyeji Uganda katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa mwishoni mwa wiki, ikishinda 4-1. Mabao ya Kili yalifungwa na Donosia Daniel, Mwanahamisi Omari, […]

Azam majeruhi, hasira zote kwa Ndanda

NA SALMA MPELI, KIKOSI cha Azam kinatarajiwa kuifuata Ndanda FC Alhamisi hii, huku wakiwa na hasira za kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo baada ya kupoteza mechi yao iliyopita dhidi ya Simba. Jumamosi iliyopita, Azam walikuwa wenyeji wa Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru na timu hiyo kukubali kichapo cha bao 1-0. Akizungumza na […]

Kichuya aamsha hisia mpya Simba

NA ZAITUNI KIBWANA, KITENDO cha winga wa Simba, Shiza Kichuya, kwenda kushangilia bao alilofunga dhidi ya Azam FC kwenye bango lililokuwa na picha ya Patrick Mafisango, kimeamsha hisia mpya ndani ya klabu hiyo. Kichuya alifunga bao lililoipa Simba ushindi wa bao 1-0 katika mchezo huo dhidi ya Wanalambalamba hao na kukaa kileleni, mchezo uliochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita Uwanja wa […]

Simba kuoga noti Oktoba mosi

NA MAREGES NYAMAKA, ACHANA na fedha kiduchu za madafu ambazo wachezaji wa Simba wamekuwa wakipewa kila timu yao inapoibuka na ushindi kutokana na utaratibu uliowekwa na vigogo wao, kufuru zaidi ya noti inatarajiwa kufanyika Oktoba mosi iwapo Wekundu wa Msimbazi hao watawaliza Yanga. Simba wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na pointi 13, baada ya mwishoni mwa wiki […]