Deschamps kocha mpya Juventus?

TURIN, Italia DIDIER Deschamps ameibuka mstari wa mbele katika orodha ya makocha wanaotakiwa kwenda kukalia kiti cha Massimiliano Allegri pale Juventus. Deschamps licha ya kuichezea, pia aliwahi kuinoa Juve, akibeba mara mbili mfululizo taji la Serie A. Ni miezi michache tu imepita tangu Deschamps mwenye umri wa miaka 50 alipoipa Ufaransa ubingwa wa Kombe la Dunia. Curry aongoza mauaji Warriors […]

Mourinho atajwa Man United

MANCHESTER, England JINA la Jose Mourinho limeibukia Old Trafford kama utani na hiyo ni baada ya kiungo anayesepa zake, Ander Herrera, kusema kocha huyo hakuwa tatizo wakati timu hiyo ilipokuwa ikifanya vibaya. Kwa anavyoona yeye, wachezaji wanapaswa kubebeshwa lawama kwa asilimia 75 ya kile kilichoikuta Man United, hata kugharimu kibarua cha mkufunzi huyo. Herrera aliongeza kuwa Mourinho raia wa Ureno […]

NDIYE YEYE BWANA…Adui wa Neymar apewa rungu Liver, Tottenham zikiuana fainali Uefa

LONDON, England ZIKIWA zimebaki wiki mbili na siku 16 kabla ya mtanange wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya Liverpool na Tottenham, jana Shirikisho la Soka barani humo (Uefa) lilimtaja mwamuzi Damir Skomina kuwa ndiye atakayekuwa katikati ya uwanja. Wasaidizi wake ni Jure Praprotnik, Robert Vukan, huku Antonio Mateu Lahoz akiwa mwamuzi wa akiba, wakati wale watakaokuwa wakiufuatilia […]

Yanga Princess kurudi kivingine msimu ujao

NA GLORY MLAY WAKATI Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake Tanzania ikifikia ukingoni, Kocha wa Yanga Princess, Khamis Kinonda, amesema wanajipanga kwa msimu ujao baada ya kushindwa kuchukua ubingwa msimu huu. Akizungumza na BINGWA jana, Kinonda alisema malengo yao yalikuwa ni kuchukua ubingwa msimu huu lakini wameshindwa kutokana na ushindani. Kinonda alisema timu yake ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza […]

Azam FC kuanza mawindo ya Mtibwa Sugar leo

NA ZAINAB IDDY BAADA ya kushindwa kulipa kisasi kwa Simba, kikosi cha Azam FC leo kinaingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar. Azam FC iligawana pointi moja na Simba, Uwanja wa Uhuru na kushindwa kulipa kisasi cha mabao 3-1, waliyofungwa Uwanja wa Taifa mzunguko wa kwanza wa ligi. Akizungumza na BINGWA, Mratibu wa Azam […]

Aron Karambo anukia Yanga

NA TIMA SIKILO KIPA wa timu ya Tanzania Prisons, Aaron Karambo, amehusishwa na kusajiliwa ndani ya kikosi cha Yanga kuelekea katika usajili wa wachezaji Ligi Kuu Tanzania Bara. Awali, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Adolph Rishard, alidai anahitaji kusajili golikipa wa ndani ambaye anafanya vizuri. Kigogo mmoja wa Yanga aliliambia BINGWA kuwa, inaonekana dhahiri kwamba viongozi wanamtaka Karambo. Alisema bado […]

Kigogo TRA aula Yanga

NA WINFRIDA MTOI ALIYEWAHI kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi uliopita wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Shija Richard, ameteuliwa kuwa mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga. Richard ambaye ni mtumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ni kati ya wajumbe wawili walioteuliwa na Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla, mwingine akiwa ni Athuman Kihamia ambao wataungana na […]

KISA POINTI 8…SIMBA WAITISHA KIKAO KIZITO 

Kuivaa Mtibwa wakiwa na harufu ya ubingwa ZAITUNI KIBWANA NA HUSSEIN OMAR KITENDO cha kufungwa na Kagera Sugar na kutoka sare dhidi ya Azam FC, kimewashtua mabosi wa Simba na kuamua kuweka kikao kizito kupanga mikakati ya ushindi wakianza na mchezo wa leo watakapoivaa Mtibwa Sugar. Simba inavaana na Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaopigwa Uwanja […]

YANGA YA KARNE

Kusajili vifaa hatari kuwakomesha Coulibaly, Chama, Kagere, Okwi Zahera akwea pipa kumalizana na aliowapigia simu Akina Lunyamila, Mmachinga, Mayay wapewa shavu ‘bab kubwa’ WINFRIDA MTOI NA TIMA SIKILO MAMBO yamezidi kunoga Yanga kuhusiana na suala zima la usajili, ambapo uongozi wa klabu hiyo umesisitiza kutotaka masikhara katika mchakato huo, mkakati wao ukiwa ni kunasa wachezaji watakaounda kikosi cha karne. Achana […]