Kinda wa Dallas Mavericks aishangaza Houston Rockets

DALLAS, Marekani NYOTA wa timu ya kikapu ya Dallas Marvericks inayoshiriki Ligi Kuu ya NBA, Luka Doncic, usiku wa kuamkia jana aliwaongoza wenzake kuitandika Houston Rockets kwa pointi 107-104. Doncic mwenye umri wa miaka 19, alimaliza mechi hiyo kwa kufunga pointi 21 na ‘rebounds’ saba, kiwango kilichodhihirisha kuwa kinda huyo sasa ameimarika kwa ajili ya kupambana NBA.

Joshua awaita ulingoni Wilder, Tyson Fury

LONDON, England BINGWA wa masumbwi uzito wa juu mikanda ya WBA, IBF na WBO, Anthony Joshua (22-0), yupo tayari kuzichapa na wababe wenzake, Deontay Wilder na Tyson Fury, hiyo ni kwa mujibu wa promota, Eddie Hearn. Hearn alisema, Joshua kwa sasa anamtaka Wilder ulingoni lakini kama atamkosa mbabe huyo raia wa Marekani, basi atahamia kwa Mwingereza mwenzake, Fury. Ikumbukwe Wilder […]

Borussia Dortmund ni jogoo aliyegoma kufa kwa utitiri

UNAIONA Borussia Dortmund? Halafu iangalie na Bayern Munich. Msimu huu wanapishana kwa kiasi kikubwa. Mmoja yupo juu, mwingine chini. Aliye chini alishazoea vya juu na anayetamba kileleni aliteseka chini. Dortmund inafanya makubwa msimu huu kwenye Bundesliga, ikionesha makali yao hasa katika eneo la mashambulizi lenye nyota watano wanaotisha zaidi kwa sasa wakiongozwa na nahodha wao, Marco Reus. Wanaoshirikiana vyema na […]

Kati yatimu hizi ipi itatinga 16 bora Uefa

 LYON, Ufaransa  MPAKA sasa timu 12 zimeshajihakikishia kucheza hatua ya 16 bora ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na nyingine nne zinaweza kuungana nazo na huku nane zikitarajiwa kushuka katika Ligi ya Europa hatua ya 32 bora. Timu ambazo zimeshajihakikishia hatua hiyo ya 16 bora ni Ajax, Atlético Madrid, Barcelona, Bayern Munich, Borussia Dortmund, Juventus, Manchester City, Manchester United, […]

Alba:Huyo Pele vipi?

 MADRID, Hispania BEKI wa Barcelona, Jordi Alba, ameshangaa nyota wa zamani, Pele kwa kumponda staa wao, Lionel Messi na huku akisema kwamba tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa dunia, Ballon d’Or, inatolewa kwa uongo.  Katika hali ya kushangaza, Messi alijikuta akishika nafasi ya tano katika kinyang’anyiro hicho cha kuwania tuzo hiyo ya Ballon d’Or ambayo aliitwaa nyota wa Real […]

Mkaliwa Simba aliyepewa heshima ya Yanga

NA HENRY PAUL KATIKA kumbukumbu za wapenzi wa soka nchini, kuna ambao wanajiuliza sababu za baadhi ya nyota waliotamba nchini kupachikwa majina kadha wa kadha mbali ya yale ya kuzaliwa. Miongoni mwa wachezaji wa zamani ambao waliwahi kupachikwa majina ya ziada, yupo aliyekuwa nyota wa kikosi cha Simba na timu ya taifa, Taifa Stars, Deo Njohole. Unafahamu mkali huyo ambaye […]

Aussems: Nitawaua hivi Nkana

NA HUSEIN OMAR KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amesema falsafa waliyoitumia ugenini ya kushambulia mwanzo mwisho na kufanikiwa kupata ushindi dhidi ya Mbabane Swallows ya Swaziland, ndiyo watakayoitumia watakapocheza na Nkana FC wiki ijayo mjini Lusaka, Zambia. Simba itavaana na Nkana katika mchezo huo wa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ikiwa ni siku chache baada ya […]