Rooney akamatwa akiwa ‘tungi’

NEW YORK, Marekani STRAIKA Wayne Rooney amethibitisha kukamatwa katika uwanja wa ndege mjini Virginia, nchini Marekani, siku 10 kabla ya Sikukuu ya Krismasi kwa tuhuma za ulevi. Mwanasoka huyo mwenye umri wa miaka 33, alisema kuwa alikamatwa kabla ya siku hizo 10 akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Washington Dulles na kutozwa fainali ya dola 25, lakini akasema […]

Bieber na mkewe ni bata kwa kwenda mbele

NEW YORK, Marekani MWANAMUZIKI mahiri, Justin Bieber na mkewe, Hailey Baldwin, bado wanaendelea kula bata katika fungate yao licha ya kuwa walifunga ndoa miezi michache iliyopita. Kwa mujibu wa gazeti la Metro, mwishoni mwa wiki wawili hao walikuwa kwenye ufukwe wa Santa Monica, uliopo mjini California ambapo  Hailey amepigilia koti refu na suruali ya jinzi na huku JB akiwa ametinga […]

Nicki Minaj aweka njiapanda mashabiki wake

NEW YORK, Marekani STAA Nicki Minaj amewaacha njiapanda mashabiki baada ya kuibua tetesi zinazodai kwamba huenda ni mjamzito na tayari ana jina la mwanawe kichwani.  Kwa sasa rapa huyo yupo kwenye penzi zito akiwa na mpenzi wake mpya, Kenneth Petty, ambaye alimtangaza mwishoni mwa mwaka jana.  Na sasa baada ya kutesa naye katika sikukuu za mwaka mpya, mwimbaji huyo anasemekana […]

Mitandao isiwape kiburi wasanii wenye mashabiki wengi

CHRISTOPHER MSEKENA NIANZE kwa kusema nimekutana na kauli za wasanii wakubwa hapa Bongo na nje  wakitamba kuwa katika kipindi hiki cha mitandao ya kijamii, vyombo vya habari kama vile redio, runinga, magazeti havina nguvu tena ya kutangaza kazi zao za sanaa. Hatua hiyo imekuja kutokana na ukweli kwamba katika mitandao ya kijamii, wasanii wamekuwa na mashabiki wengi hivyo kurahisisha masuala […]

Makambo avalishwa viatu vya Msuva

WINFRIDA MTOI MCHAMBUZI wa soka hapa nchini na mchezaji wa zamani wa Yanga, Ally Mayay, amemfananisha mshambuliaji, Heritier Makambo na kiungo, Simon Msuva, kutokana kuendelea kupanda kwa kiwango chake na kuwa tishio. Makambo aliyetua Yanga kuitumikia kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, tayari ameifungia timu hiyo mabao 11 katika mechi 18 alizocheza huku akitwaa tuzo ya mchezaji bora wa […]

Kaheza kurudi kuivaa Simba SportPesa Cup

MWANDISHI WETU MABINGWA wa Ligi Kuu Bara, Simba, wataanza kampeni yao ya kusaka taji la SportPesa watakapowavaa AFC Leopards ya Kenya Januari 23 mwaka huu Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Itakuwa ni mara ya kwanza kwa mshambuliaji wa Simba, Marcel Kaheza, anayekipiga kwa mkopo AFC Leopards ya Kenya kurudi nchini kuivaa timu yake ya zamani.  Kabla ya mechi […]

Zahera: Miezi miwili tu Yanga tajiri

HUSSEIN OMAR HII inaweza kuwa habari njema kwa mashabiki wa Yanga baada ya kocha mkuu wao kipenzi, Mwinyi Zahera, kutamka wazi kwamba anaweza kuifanya klabu hiyo kumaliza ukata wa kifedha ndani ya miezi miwili kutokana na hazina kubwa ya wanachama na mashabiki iliyonayo. Yanga ni klabu kongwe nchini, lakini imekuwa ikishindwa kutumia rasilimali ilizonazo katika kujiletea maendeleo, huku baadhi ya […]

Jjuuko apewa mikoba ya Nyoni

*Beki huyo kiraka arejeshwa Dar kwa vipimo *Vigogo Simba, serikalini wapata mshtuko SAADA SALIM, ZANZIBAR KOCHA Mkuu wa Simba, Mbelgiji Patrick Aussems, ameanza kumwandaa beki wake, Jjuuko Murushid, kuchukua nafasi ya Erasto Nyoni, ambaye hatakuwepo katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya JS Saoura ya Algeria Jumamosi ya wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Nyoni ameondolewa […]

Rayvan aishukuru Basata, kuruhusu WCB kufanya matamasha nje ya nchi

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam Rayvan aishukuru Basata, kuruhusu WCB kufanya matamasha nje ya nchi Msanii wa Bongo Fleva kutoka lebo ya WCB, Raymond Mwakyusa maarufu Rayvanny amelishukuru Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kuruhusu yeye na wasanii wenzake kutoka lebo hiyo kufanya Tamasha la Wasafi Festival katika miji ya Mombasa, Nairobi na nchini Comoro ambapo awali walizuiliwa. Desemba […]

Tajiri wa masikini- 76

Ilipoishia  “Samahani kwa kosa langu najua unafahamu nilifanya vile kwa sababu gani Vanuell. Najua unatambua fika jinsi gani moyo wangu unavyopata tabu juu yako.”  “Hayo yalishapita Lucy yafaa tutazame yajayo,” nilimwambia.  “Nashukuru kwa kunisamehe na kumfanya Theresa anisamehe pia, lakini pamoja na yote hayo bado naumia sana juu yako na sijui nifanye nini?” SASA ENDELEA… “HUNA la kufanya Lucy kwa […]