Msuva, Ulimwengu waongoza tizi Stars

NA MWAMVITA MTANDA WACHEZAJI 18 wa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, wameanza mazoezi jana kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon 2019) dhidi ya Uganda utakaochezwa Machi 24, mwaka huu. Katika mazoezi hayo, wachezaji wa kimataifa waliofika ni Simon Msuva anayechezea timu ya Difaa El Jadid ya nchini Morocco na […]

Paul Mashauri ataoa siri ya Mwamba Wangu

NA MWANDISHI WETU MWIMBAJI wa nyimbo za Injili nchini, Paul Mashauri, ameumeutoa video ya wimbo, Mwamba Wangu kwaajili ya Pasaka  huo kwajili ya Pasaka baada ya kupata maono ya kuandika wimbo huo mwanzoni mwa mwaka huu. Akizungumza na Papaso la Burudani, Paul alisema alipata ufunuo usiku na alipoamka asubuhi akamshirikisha mke wake ambaye alimtia moyo kwa kumwambia huo siyo wimbo […]

Meek Mill atengewa siku za mapumziko

MPHILADELPHIA,MAREKANI RAIS wa Halmashauri ya Philadelphia nchini Marekani, Darell L Clarke, ametangaza kuwa Machi 14 mpaka 17 ya kila mwaka zitakuwa ni siku za mapumziko  yaani Meek Mill Weekend kwa wakazi wote wa mji huo. Hatua hiyo imekuja baada ya rapa Meek Mill, kuupa heshima kubwa mji huo ikiwamo kutetea wafungwa mpaka sheria za adhabu kwa wafungwa kubadilishwa. Mapema mwezi […]

Rosa Ree awang’ata sikio vijana

RNA MWANDISHI WETU BAADA ya kuwaonyesha mashabiki gari lake jipya aina ya BMW, rapa wa kike Rose Ree amewataka vijana kufanya kazi kwa bidii hata kama wanapitia changamoto zinazowakatisha tamaa. Akizungumza na Papaso la Burudani, Rose Ree ambaye anafanya vizuri na wimbo Asante Baba alisema anashukuru mashabiki wameendelea kumpa sapoti ya nguvu na mafanikio yameanza kuonekana. “Napenda kuwaambia vijana kwamba […]

Minziro ashindwa kuvumilia muziki wa Niyonzima

NA WINFRIDA MTOI VITU adimu alivyofanya kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima, katika mchezo wa  marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), vilimfanya kocha msaidizi wa zamani wa Yanga, Fred Minziro kushindwa kuvumilia na kujikuta akishangilia. Mchezo huo uliochezwa juzi  kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam,  Simba walishinda 2-1 […]

Makambo aiponza Yanga Iringa

KOCHA Mkuu wa Lipuli FC, Samwel Moja, amefichua siri ya kilichoimaliza Yanga kuwa ni kuzoea mfumo wa kumtegemea zaidi Heritier Makambo, kufunga mabao. Lipuli juzi iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Samora, Iringa.  Akizungumza na BINGWA jana, kocha huyo alisema alikuwa akiifuatilia Yanga kwa muda mrefu […]