Pochettino: Mlituchukulia poa Uefa

LONDON, England MKUU wa benchi la ufundi la Tottenham, Mauricio Pochettino, amesema hakuna aliyekuwa akiipa timu yake nafasi lilipokuja suala la timu zitakazofika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ikiwa imepangwa kundi lililokuwa na PSV, Inter na Barcelona, Tottenham waliingia hatua ya mtoano wakishika nafasi ya pili, ikichangiwa na sare yao dhidi ya Barca katika mchezo wa mwisho. “… […]

Liverpool watamba kuizima Barca

LONDON, England KAMA huipendi Liverpool basi tambua utapata tabu sana, kwani Barcelona wataambulia kichapo tu pale Anfield kwa mujibu wa James Milner, kuelekea mchezo wao wa siku 11 zijazo. Mtanange huo utatanguliwa na ule wa Tottenham na Ajax, ambao utachezwa Aprili 30 jijini London kabla ya ule wa marudiano kule Uholanzi. Liverpool ni tofauti na Machester United iliyotolewa na Barca […]

Uchaguzi Mkuu Yanga… Waliokatwa waitwa

NA ZAITUNI KIBWANA SIKU chache baada ya wagombea wa nafasi za ujumbe katika Uchaguzi Mkuu wa Yanga, Hussein Nyika na Sumuel Luckumay kuenguliwa kwenye mchakato huo, Kamati ya Uchaguzi ya timu hiyo imetangaza wote waliopigwa panga kwenda kukata rufaa. Nyika, Luckumay, Thobias Lingalangala pamoja na Siza Limo ni kati ya waliopigwa panga kwenye uchaguzi huo baada ya kuwekewa pingamizi linalotokana […]

Kagere aahidi ushindi Kaitaba

NA HUSSEIN OMAR MSHAMBULIAJI wa Simba, Meddie Kagere, ameahidi kuwa wataendeleza wimbi la ushindi katika mchezo wao mwingine wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa leo kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba. Simba watacheza mchezo huo baada ya kutoka kuwachapa Coastal Union 2-1 katika mtanange huo uliopigwa katikati ya wiki kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, ambapo Kagere […]

Lulu Diva, Wakazi hapatoshi Kigamboni mkesha wa Pasaka

NA MWANDISHI WETU KATIKA kusherehekea mkesha wa Sikukuu ya Pasaka, mamia ya mashabiki wa Bongo Fleva wanaoishi Kigamboni, Dar es Salaam, wanatarajia kupata burudani ya nguvu kutoka kwa Lulu Diva na rapa Wakazi. Mratibu wa onyesho hilo, Mbwana Khamis, alisema wasanii hao watadondosha burudani katika klabu ya usiku ya Jembe One kuanzia saa mbili usiku na kuendelea. “Mbali na Lulu […]

Wanachama, hii ni nafasi yenu ya mwisho kuiokoa Yanga

NA HUSSEIN OMAR KAMPA kampa tena! Wakimataifa, Watoto wa Jangwani na Wazee Ndege! Ni baadhi tu ya majina ambayo Klabu ya Yanga ilibatizwa miaka kadhaa iliyopita, kabla ya hali ya sasa inayowakumba mithili ya kupigania uhai wake. Kutoka kuyasikia majina hayo mpaka kubatizwa mengine kama Wazee wa Bakuli, Chura Churani, Omba Omba FC, Wazee wa Buku, si jambo zuri hata […]

Mfalme Neymar anapokimbia ngome zake taratibu

NA AYOUB HINJO KADIRI siku zinavyosogea kupisha jua kuchomoza na kuzama kisha mwezi kuchukua nafasi yake kumulika anga wakati wa kiza kinene, kuna mambo mengi hutokea katika uso wa dunia hii tunayoishi ndani yake. Ndivyo ilivyo katika maisha yetu ya kila siku ambayo yamekuwa hayaeleweki kwa baadhi ya watu, huku kwa wengine yakionekana kwenda sawa kama kupiga mstari mnyoofu na […]

‘TRA’ wamshukia Diego Costa 

MADRID, Hispania MAMLAKA zinazoshughulika na masuala ya kodi nchini Hispania, zimemtia hatiani straika wa Atletico Madrid, Diego Costa, kwa madai ya ukwepaji kodi. Imedaiwa kuwa mpachika mabao huyo wa Atletico, alilipwa kiasi cha euro milioni moja kwa njia isiyofaa mwaka 2014 aliposajiliwa na klabu ya Chelsea. Kwa mujibu wa ripoti ya kodi, malipo hayo yalifanyika tofauti na kiasi cha awali […]