P-SQUARE INAWEZA KURUDI UNAAMBIWA

LAGOS, Nigeria


ENDAPO kile anachokitaka Peter Okoye kitafanyika, basi mashabiki wa Kundi la P-Square wajiandae kulishuhudia likirejea katika ubora wake.

Kundi hilo lilivunjika baada ya Peter na kaka yake Paul kukorofishana, ikifikia hatua ya mapacha hao kutupiana maneno makali katika mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, Peter anaamini P-Square itarejea endapo baadhi ya watu wa karibu wa kundi hilo wataiheshimu familia yake.

“Kundi limevunjika mara tatu na tatizo lilikuwa hilohilo. Hivyo, kama tunataka lirejee, basi suluhisho lipatikane kwanza. Psquare inaweza kurudi au isirudi,” alisema.

Peter alisisitiza kuwa mke na watoto wake ni kitu cha msingi zaidi, hivyo hawezi kuona wakidhalilishwa kisa muziki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*