OXLADE-CHAMBERLAIN: NAENDELEA VIZURI

MERSEYSIDE, England


 

KIUNGO wa timu ya Liverpool, Alex Oxlade-Chamberlain, amesisitiza kuwa ana matumaini makubwa ya kupona jeraha lake la goti kwani anaendelea vizuri.

Nyota huyo huenda asionekane dimbani msimu huu kufuatia kuumia sehemu kubwa ya goti lake katika mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita dhidi ya AS Roma.

Hata hivyo, wikiendi iliyopita alihojiwa na kituo cha Sky Sports, akisisitiza imani yake juu ya maendeleo mazuri ya jeraha lake hilo.

“Niliumia vibaya sana na inaweza kumtokea yeyote muda wowote, hivyo huwa si kazi rahisi kukabiliana na hali hiyo,” alisema.

“Lakini naendelea vizuri nikiwa na mtazamo chanya.”


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*