OMOTOLA ASHAURIWA KUJIANGALIA UZITO

LAGOS, Nigeria


STAA Omotola Jalade ameshauriwa na wenzake kujiangalia uzito wake baada ya kuonekana kunenepa zaidi.

Vyanzo vya habari viliuambia mtandao wa Nollywood juzi kwamba, kwa sasa staa huyo anaonekana kuwa na uzito mkubwa kwa kile kilichodai pengine ni matumizi ya dawa za kuzuia ujauzito.

Chanzo kimoja cha habari kilieleza kuwa, matumizi ya dawa hizo yamekuwa yakiwaathiri wasanii wengi katika tasnia ya filamu za Nollywood.

“Hata si mjamzito, ninachohisi anatumia dawa za kuzuia ujauzito na hiki kimekuwa kikichangia wasanii wengi Hollywood kuongezeka uzito,” kilieleza chanzo hicho.

“Kwa mfano, hata mimi nilikumbana na jambo hilo kabla ya kuondoa kitanzi. Kilinisaidia nisipate ujauzito hadi nilipokiondoa baada ya kuona sina jinsi katika kukabiliana na mwili mwangu,” kiliongeza chanzo hicho.

Kilisema kuwa mara nyingi watu huwa hawafahamu njia wanazozitumia wanawake kuzuia ujauzito na kikasisitiza kuwa, lazima Omotola atakuwa anatumia njia hiyo ili kujizuia ujauzito.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*