Nyota Yanga aionya Simba

@@

NA ZAINAB IDDY

MCHEZAJI wa zamani wa timu ya Yanga, Ally Mayay, ameutaka uongozi wa klabu ya Simba kuwa makini katika kufanya maamuzi ya kumpata kocha atakayemrithi  Patrick Aussems.

Simba ilitangaza kuachana na Aussems  juzi kwa madai ya kushindwa kufikia malengo  waliyokubaliana.

Akizungumza na BINGWA jana, Mayay alisema Simba haitakiwi  kukurupuka  kuchagua kocha, kwani kutawaweka katika hatari ya kupoteza nafasi ya kutetea  ubingwa wao wa Ligi Kuu.

 “Ukiangalia hadi sasa Simba  ina nafasi ya kutetea  ubingwa lakini  ujio wa kocha mpya unaweza kuvuruga jambo hilo hasa akiwa mgeni na soka la Tanzania.

“Kutokana na ukubwa wa klabu ya Simba, wanaonekana kuwa na malengo makubwa kimataifa, hivyo wanapaswa kumleta kocha mwenye uwezo wa juu zaidi ya Aussems lakini pia awe na uelewa wa haraka la soka la Tanzania”.

Mayay aliongeza: “Kama watafanya mamauzi kwa kufuata upepo kwa maana ya kukurupuka wanaweza kuiweka nafasi yao ya  kutetea ubingwa  hatarini . Katika msimamo wahiyo, Simba inaongoza ikiwa na alama 25 baada ya kucheza mechi 10, imaeshinda nane, sare moja na kupoteza mmoja


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*