googleAds

Nyota Mbeya City watakiwa kupambana

NA ZAINAB IDDY

KOCHA wa Mbeya City, Amri Said, amesema  wachezaji wake wanatakiwa kucheza soka ya ushindani na kuiwezesha kushinda.

Mbeya City  inashika  nafasi ya pili kutoka mkiani  kutokana na pointi 14, baada ya kucheza michezo 19.

Akizungumza na BINGWA jana, Amri alisema mzunguko wa pili wa ligi hiyo ni mgumu zaidi kwa sababu kila timu inaingia uwanjani kwa lengo la kupata matokeo mazuri.

“Kama ambavyo sisi tunahaha kutafuta namna ya kubaki ligi,  ndivyo kuna wengine nao wanahangaika hivyo hivyo, jambo hili litatupa wakati mgumu kupata alama tatu.

“Lakini licha ya ukweli juu ya ugumu uliopo nalazimika kupambana kadri niwezavyo ili kuiwesesha timu kucheza soka la ushindani litakalotupa pointi tatu katika kila mechi tutakayocheza ili iweze kubaki ligi,” Amri.

Mbeya City inatarajiwa kuchezwa na  Tanzania Prisons katika mchezo utakochezwa leo kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*