googleAds

Nyota Mbeya City wamfurahisha Amri

NA WINFRIDA MTOI

KOCHA wa timu ya Mbeya City, Amri Said, amesema kikosi chake kimeanza kubadilika kwa kiasi kikubwa, anachosubiri ni matokeo ya kushinda uwanjani.

Amri alikabidhiwa kikosi hicho, baada ya Juma Mwambusi kujiuzulu kutokana na matokeo mabaya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na BINGWA jana, Amri  alisema baada ya kufanya usajili katika dirisha dogo, timu imeonyesha mabadiliko katika mechi walizocheza.

Amri alisema moja ya  mafanikio yaliyotokana na usajili mpya ni kusonga mbele katika michuano ya Kombe la FA, maarufu michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC), baada ya kuitoa Polisi Tanzania.

“Nashukuru timu yangu imebadilika si kama nilivyoichukua kipindi cha nyuma, hilo nileiona katika mechi tulizocheza  na ninachosubiri ni matokeo tu uwanjani,” alisema.

Kocha huyo alisema kazi kubwa anayofanya ni kujaribu kutengeneza muunganiko mzuri zaidi wa wachezaji baada ya kubaini hawakuwa na uzoefu wa kucheza Ligi Kuu Bara.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*