googleAds

Nyota Madrid nje miezi saba

download (4)

MADRID, Hispania

MCHEZA kikapu wa timu ya Real Madrid inayoshiriki ligi ya mchezo huo Hispania, Liga ACB, Sergio Llull, anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi saba baada ya kuumia vibaya goti.

Llull, alikumbwa na jeraha hilo katika goti lake la kulia alipokuwa akiitumikia timu yake ya taifa ya Hispania dhidi ya Ubelgiji katika michuano ya Eurobasket usiku wa kuamkia jana.

Staa huyo anatarajiwa kukosa michuano hiyo ya kimataifa sambamba na msimu mpya kwa timu yake ya Real Madrid.

Wacheza kikapu wengi wamekuwa wakisumbuliwa sana na maumivu ya goti, na kwa jinsi alivyoumia Llull, itamchukua muda mrefu kupona kwani ni jeraha kubwa.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*