NYIE YANGA MBONA MMERUDI MAPEMA KAMA KIFURUSHI CHA SIKU KWENYE SIMU?


HIVI kweli walifikisha hata saa 72 kule Kenya jamani? Sina hata uhakika, yaani ina maana hii mimaji na misabuni niliyonunua sitaweza kufua ile mijezi yao.

Khaa! Nilitegema kidogo wangesogeasogea hata hatua moja mbele, sasa tunafanyaje ikiwa hali yenyewe kila mmoja ameiona.

Sasa na hicho kipigo lawama tumpe nani tena? Yaani kabisa nilitegemea wachezaji kule wangejituma weee ili wapate timu za kuwanunua lakini kwa kiwango kile walistahili kutoka tu.

Tatizo wametoka kirahisi sana. Teh teh teh unajua ukitaka kuwahi kwenda mbinguni kwa haraka zaidi, pita pale mitaa ya Jangwani halafu taja jina la Alan Wanga, utafikishwa haraka tu unapopataka kwenda.

Hata mitaa hawaijui masikini yao jamani, zaidi ya hoteli waliyofikia na njia ya kuelekea uwanjani tu, dah! Kweli Wanga hafai asee.

Ngoja nimpigie Joji simu, niachane na sitresi zenu asee… maana nasikia Joji alipokelewa kifalme huko, karudi homu… teh teh teh alikuja chibonge, lakini amerudi mwembambaa.. kwani Joji alikuwa hali jamani?

Halooo Joji… vipi huko unaendeleaje asee? Aaah kweli au unanitania, yaani ukiamka tu kuku.. ukikaa kidogo juisi, kwa maana hiyo lengo lao wakurudishie mwili wako… vizuri sana, huku tumekumiss sana, maana tangu uondoke tumefanikiwa kushinda mchezo mmoja tu.

Sasa Joji niambie ukweli… kwani wewe ulikuwa unashindaje mechi zako asee? Kwani wachezaji si hawahawa? Na wenzako kwenye benchi si walewale?

Yaani umeondoka wewe tu Joji! Majanga makubwa yametokea, teh teh teh maana hadi jina limebadilika siku hizi wanaitwa ‘mahandaki fc’.

Aah! Aah! Hapo 0umeongea Kiingereza cha ndani sana… taratibu mzee, kwani kilichokukimbiza ni njaa au kulikuwa na vingine mzee?

Maana ungekuwepo haya yote yasingetokea asee, hadi Kakamega wa kuifunga Yanga? Teh teh teh basi rudi na wewe hata kwa bahati mbaya tu.

Hata yule msaidizi wako anayenyoa upara simuoni kabisa pale kwenye benchi, kuondoka kwako kila kitu kimebadilika asee, mambo hayaendi vizuri kabisa.

Joji eeeeh kuwa siriaz sasa, unarudi au haurudi? Maana hata yule Zahera haonekani, tangu alivyoaga anaenda kwenye majukumu ya taifa hapatikani.

Unajua ile michuano ya kule Kenya ilikuwa njia pekee ambayo niliamini ningefua mijezi yao hadi mikono ichubuke, lakini haikuwa hivyo.

Wamerudi mapema sana kama bando la siku tu, sasa kilichobaki ni kutupiana lawama tu, wamezikosaje zile milioni 60 za kule?

Wangepambana kwa nguvu pesa zile zingesaidia kidogo katika matatizo ambayo yapo ndani ya timu hiyo.

Lakini ndio hivyo wameshindwa kuendelea bhana, sasa kilichobaki hii mimaji ambayo niliiandaa kufua mijezi yao inabidi niitunze vizuri maana najua bado wana michezo ya kimataifa.

Ndio bado wanapanda ndege bhana, sasa kama wasipojipanga vizuri tena watapigwa vipigo vya mbwa koko.

Maana watu wapo siriaz bhana, wajitahidi hata kidogo basi kuendana na ule moto wao wa ‘nyuma mwiko, daima mbele’.

Kwa kuwa bado muda wa kujiandaa upo hata mimi nawasubiri tu, sitaki sitresi kwa sasa maana wamenivunja moyo.

Sijui ndugu yangu Ally Kamwe yupo na hali gani huko Kenya? Hali si hali acha nimjibie tu, juzi peke yake timu mbili za TZ zimetolewa.

Sasa hawa masharubu nao sijui vipi? Sitaki kabisa presha wala sikuwaangalia wala kuwasikiliza, leo hawa Singida United nao sijui itakuaje?

Hawa Wakenya wakishinda michezo yote itakuwa aibu sana, kwa jinsi nilivyoifua mijezi yao wakati wanapanda ndege sikutegemea wengine kutolewa mapema kama vifurushi vya siku vya mitandao ya simu.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*