googleAds

Nonga atua Malaysia kufanya majaribio

NA WINFRIDA MTOI

MSHAMBULIAJI wa Lipuli, Paul Nonga, ametimkia Malaysia kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini humo.

Nonga ambaye ni nahodha wa kikosi hicho,  ameanza vizuri msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, akifunga mabao nane.

Kaimu kocha mkuu wa Lipuli, Julio Elieza, aliliambia BINGWA kuwa mchezaji huyo aliondoka wiki iliyopita na endapo atakamilisha program yake atarejea nchini wiki ijayo.

Elieza alisema hana tatizo kumkosa mchezaji huyo kwa sababu amekwenda kufanya kitu kizuri ambacho kinakuwa na manufaa kwa timu na soka la Tanzania kwa ujumla.

“Mchezaji wetu Nonga yupo Malaysia anafanya majaribio na ndiyo sababu haonekani kikosini, ni jambo jema kwetu na tunamuombea afanikiwe ili kuipa heshima timu yetu.

“Nampa baraka zote mchezaji wangu huko aliko aweze kufanikiwa, najua itakuwa njia ya wengine kutoka,”alisema.

Elieza alisema japo ni pengo kubwa kwao kumkosa nyota huyo, ukizingatia ni nahodha wa timu, lakini atajitahidi kutumia wengine waliopo kuliziba.

Lipuli inatarajiwa kukutana na Mbeya City kesho kwenye dimba la Samora, mkoani Iringa


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*