Ninja awapoza mashabiki Yanga

NA ZAITUNI KIBWANA

BEKI wa Yanga, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, amewataka mashabiki wa timu hiyo kutokuwa na wasiwasi, kwani kikosi chao kitarekebisha makosa na kufanya vizuri.

Ninja amesema hayo baada ya timu hiyo kuchapwa bao 1-0 na Mtibwa Sugar, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Akizungumza na BINGWA jana, Ninja alisema mashabiki wa Yanga waendelee kuwa wavumilivu, kwani wanapambana kwa ajili ya timu hiyo.

“Naomba mashabiki wetu waendelee kuwa wavumilivu, kwani  wenyewe wanaona tunavyopambana na hata wanachotufanyia waamuzi,” alisema Ninja.

Alisema kwa sasa matokeo dhidi ya Mtibwa Sugar wameshayasahau na akili zao wamezielekeza kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Azam, ambao utachezwa Aprili 29, mwaka huu.

“Mpira ni mchezo wa makosa, ukifanya kosa moja wenzako wanakuadhibu, ila naamini benchi la ufundi limeona na tutafanyia kazi, ila kikubwa tunaendelea kuvumilia wakati tunazidi kupambana,” alisema.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*