googleAds

  NEYMAR KUISHTAKI BARCA FIFA

PARIS, Ufaransa

MWANASOKA ghali zaidi duniani, Neymar Jr, ameripotiwa kuishtaki timu yake ya zamani ya Barcelona katika Shirikisho la Soka la kimataifa (Fifa), kwa kile anachodai ni kutolipwa baadhi ya fedha zake.

Staa huyo Mbrazil ambaye ameweka rekodi ya kusajiliwa kwa bei ghali na usajili wake kukamilika hivi karibuni  baada ya Barcelona kupokea kitita cha Euro milioni 222 kutoka kwa miamba ya Ufaransa, PSG, anasema klabu yake hiyo ya zamani ilitoa uthibitisho wa maandishi  kuwa hawatamlipa baba yake Neymar kiasi cha Euro milioni 23 ambayo ni fedha aliyotakiwa kulipwa baada ya kuongeza mkataba msimu uliopita kutokana na kushindwa kuelewana kwenye mkataba uliovunjwa ambao ulikuwa na masharti.

Chanzo cha habari cha Skysports kinasema mchezaji huyo amejisikia vibaya sana kutokana na mgogoro huo na timu yake ya zamani na kwamba  mawakili wake wanajiandaa kupeleka nyaraka zao kwenye mamlaka ya soka duniani, Fifa.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*