NEYMAR, COUTINHO KUMBE WAPO KIMWILI TU KATIKA KLABU ZAO

LONDON, England

 WACHEZAJI nyota, Neymar  na Coutinho, ndio kwa kiasi kikubwa waliweza kutawala katika habari za usajili msimu huu.

 Katika habari hizo, nyota hao walikuwa wakihusishwa na klabu mbalimbali kubwa Ulaya, kabla ya Neymar kutua kwenye klabu ya Paris Saint Germains.

 Hata hivyo, pamoja na kujiunga na klabu hizo, kumbe vinara hao unaweza kusema kuwa wapo kimwili, lakini roho na ndoto zao ni kuchezea Real Madrid.

 Kwa sasa Neymar, ambaye aliitema Barcelona na kwenda kijiunga na PSG, ameanza kutamba katika  michezo michache aliyoichezea timu hiyo, huku Coutinho akitajwa kuwa, huenda akawa mbadala wake katika vinara hao wa Catalan.

  Vinara hao wanatajwa kuwa ni marfiki wa karibu na kila mmoja anamfahamu mwenzake nje ndani tangu walipokutana Machi, 2008, walipoitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Brazil ya vijana wenye umri chini ya miaka 16, iliyoitwa kushiriki katika mashindano ya vijana wenye umri huo.

 Katika kipindi hicho, staa David Ruiz ndipo alipopata fursa ya kuteta nao na kila mmoja akaeleza dhamira  na ndoto zake za kutaka kujiunga na vinara hao wa Soka Hispania na Ulaya.

 “Real Madrid. Ndiyo timu bora Ulaya. Nilikuwa nikisafiri kwa baiskeli ili kumwangalia Robinho kwa njia ya televisheni. Nilikuwa nikizifuatilia kwa karibu Real Madrid na Barcelona, ndizo timu  nilizokuwa nikizipenda katika michuano ya La Liga,” hayo ndiyo yalikuwa maneno ya Coutinho.

 Coutinho anasema kuwa, alikuwa akilipenda soka la Hispania kutokana na kuwa lina wachezaji wazuri, kama vile  Robinho na Ronaldinho.

   Kwa upande wake Neymar, alisema licha ya kujiunga na  Santos akiwa na umri wa miaka saba, lakini ndoto zake zote zilikuwa ni Real Madrid.

  “Nilianza kuchezea Santos na kisha nikahamia Portuguesa Santista, kabla ya kurejea tena Santos. Nilikuwa nikimwangalia Robinho  mara nyingi katika televisheni  na nilikuwa nikijaribu kuiga jinsi alivyokuwa akiwachambua wachezaji wenzake,” alisema Neymar.

  Anasema pamoja na kuhama, lakini bado analipenda soka la Hispania, kutokana na kwamba linavutia na la kasi, huku likiwa na kiwango cha hali ya juu.

 

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*