Neymar anapatikana kwa bei chee tu!

PARIS, Ufaransa

IMERIPOTIWA PSG imeshusha bei ya kuuzwa kwa staa wao Neymar, inayodaiwa kupungua na kufikia pauni milioni 63 (sh bil.144) kumuachia mchezaji huyo.

Awali, bei ya Neymar imetajwa kuwa thamani ya pauni milioni 135 (sh bil. 309), na sasa wapo tayari kumpoteza kwa pesa hiyo ya sasa ambayo imetajwa.

Imeaminika nyota huyo ameishikiza PSG, kumwachia kurejea katika klabu yake ya zamani, ya Barcelona msimu ujao.

Mkurugenzi wa michezo wa PSG, Leornado aliliambia gazeti la  Le Parisien, wapo tayari kumuachia Neymar, endapo ofa nzuri italetwa mezani.

Naye baba wa mchezaji huyo amethitibisha sababu ya kuchelewa, kuripoti mazoezini kwa mchezaji huyo, ni  kutokana  na sababu zilizo nje ya uwezo wake.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*