googleAds

Ndayiragije: Ubingwa Chalenji utakuja Tanzania

KOCHA wa timu ya Tanzania Bara,  Kilimanjaro Stars, Etienne Ndayiragije, amesema ana matuamiani kuwa, ubingwa wa michuano ya Kombe la Chalenji(Cecafa), utatua Tanzania mwaka huu.

 Kilimanjaro Stars imeingia kambini juzi, kujiandaa na michuano hiyo, inayotarajia kuanza Desemba 7, mwaka huu, nchini Uganda.

Akizungumza na BINGWA jana, alisema yeye si kocha mkuu wa Kilimanjaro Stars pekee, timu hiyo itakuwa zaidi ikiangaliwa na Selemani Matola na Juma Mgunda.

Ndayiragije alisema  atakwenda Uganda kutazama timu zote mbili za Bara na Zanzibar, anaomba Watanzania kusapoti  vikosi vyote.

 “Uganda timu zetu zote zitakuwa ugenini, lakini bado hiyo sio changamoto kikubwa ni maandalizi  ya kwenda kushindana na kurudi na ushindi hakuna linaloshindikanaa,”alisema

Mara ya mwisho Kilimanjaro Stars waliishia nusu fainali ya michuano hiyo, huku Zanzibar Heroes wakifanikiwa kucheza fainali  dhidi ya Kenya.

Molinga  ajiweka salama Yanga

NA TIMA SIKILO

MSHAMBULIAJI wa Yanga, David Molinga, amejihakikishia kubaki katika kikosi hicho kutokana na juhudi anazoonyesha uwanjani.

Molinga alisajiliwa na Yanga, msimu huu chini kocha Mwinyi Zahera ambaye kwa sasa nafasi yake imekaimiwa na Charles Mkwasa.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya klabu  hiyo, zinasema uongozi hauna mpango wa kumuacha mchezaji huyo kutokana na kasi  yake ya kufunga.

 “Viongozi hawafikirii kumuacha Molinga, wanaamini kuna kitu kizuri anacho, akicheza mechi nyingi atakaa vizuri zaidi,”alisema.

Kwa upande wake Mkwasa, aliwahi kusema kuwa hawezi kumuacha au kumnyima nafasi mchezaji kwa sababu ya maumbile yake au uzito, anayejituma na ndiye atampa nafasi.

Molinga mpaka sasa ameshaifungia timu yake mabao manne, mawili dhidi ya Polisi Tanzania, JKT Tanzania bao 1 na Alliance FC bao 1.

@@@@@@@@@@@


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*