googleAds

Ndayiragije awatoa hofu Azam

NA TIMA SIKILO

KOCHA wa Azam, Etienne Ndayiragije, amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Triangle Unitedya Zimbabwe utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA jana, Ndayiragije alisema timu yake itafanya vizuri Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.

Ndayiragije alisema wamejipanga kufanya vizuri michuano yote ikiwa wa kesho dhidi ya Triangle United.

Alisema kwa kushirikiana na benchi la ufundi la timu hiyo, hakuna kitu kitakachoharibika, kwani mambo yatakwenda sawa.

“Siwezi kuacha kuinoa Azam uwezo wa kuwafundisha nakupata matokeo ninao wasiwe na hofu, licha ya kuwa na majukumu mengine timu ya Taifa Stars,” alisema Ndayiragije.

Ndayiragije amejiunga na Azam msimu huu, akitokea KMC ambayo ilimaliza nafasi ya nne msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*