googleAds

Ndayiragije atamba kumtoa nishai Aussems

TIMA SIKILO

KOCHA Mkuu wa Azam, Etienne Ndayiragije, ametamba kuitoa nishai Simba watakapokutana nayo katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Azam FC wameingia nchini jana jioni wakitokea Ethiopia katika mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Fasil Kenema, wakifungwa bao 1-0, hivyo kuhitaji ushindi wa zaidi ya mabao 2-0 watakaporudiana kati ya Agosi 23 na 24, jijini Dar es Salaam ili kusonga mbele.

Akizungumza na BINGWA jana, Ndayiragije alisema wamejipanga vilivyo kuhakikisha wanaifunga Simba Jumamosi.

“Tunashukuru tumerejea nyumbani salama na jukumu lililo mbele yetu kwa sasa ni mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, tunajipanga kupambana nao ili tupate ushindi,” alisema.

Juu ya mchezo wao wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika, alisema: “Tutajifua hasa ili tupate matokeo mazuri katika mchezo huo tukiwa nyumbani, kwetu ni wa kufa au kupona.”


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*