NANI MCHAWI WA LAUDIT MAVUGO PALE SIMBA?

NA EZEKIEL TENDWA

sirtendwa@gmail.com

0718769944

MWAKA juzi Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alitembelea ofisi yetu ya New Habari (2006) Ltd, ambapo kati ya mambo tuliyoyazungumza, lilikuwapo la uwezo wa mshambuliaji wao raia wa Burundi,  Laudit Mavugo.

Kauli ya Manara katika mjadala wetu ambayo naendelea kuikumbuka mpaka sasa,  ni alivyosema kwa miaka ya hivi karibuni hajawahi kushuhudia mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa kama ilivyo kwa Mrundi huyo.

Manara alikiri kwamba hakuwa akimfahamu vizuri Mavugo licha ya kuwa na jina kubwa wakati zikiwa zimeenea tetesi za Simba kutaka kumsajili, lakini baada ya kutua nchini, ofisa huyo akatamka wazi kuwa Mrundi huyo ni moto ambao utawaunguza wengi.

Ukweli ni kwamba kati yetu hakuna aliyembishia Manara, kwani kila mmoja aliona kasi aliyoanza nayo Mrundi huyo na kuwafanya mabeki wa timu pinzani kuanza kuumiza vichwa namna ya kumzuia ili asiwaaibishe, hakuwa mshambuliaji wa masihara hata kidogo.

Mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulikuwa dhidi ya Ndanda FC, uliochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ambapo alionyesha uwezo mkubwa na kupachika moja ya mabao  3-1 hapo ndipo kila mmoja akaamini kuwa Simba walikuwa wamelamba dume.

Simba walimsajili Mavugo kutokana na kile alichokuwa akikifanya nchini kwao Burundi akiwa anakipiga timu ya  Vital’O.

Alikuwa akifunga mabao mengi atakavyo na haraka sana vigogo wa Wekundu hao wa Msimbazi, wakaona wamsajili ili kuwasaidia ikizingatiwa kuwa walikuwa na hamu kubwa ya kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa misimu kadhaa.

Uwezo wa Mavugo kumiliki mpira, kasi kubwa, kutoa pasi za uhakika na kupiga mashuti ya maana kulianza kuwaaminisha mashabiki wa Simba akiwamo Manara kwamba wamelamba dume, lakini sasa mambo yamebadilika kwa kiasi kikubwa kwani Mavugo wa jana sio wa leo.

Kila anapopewa nafasi haonyeshi kubadilika na badala yake amekuwa akiporomoka kila kukicha.

Binafsi nilidhani kwamba hii michuano ya Mapinduzi inayofanyika Zanzibar, labda angekuja na kitu tofauti lakini ndiyo kwanza anazidi kuonyesha udhaifu kwani hata katika mchezo uliopita Simba walipoifunga Jamhuri mabao 3-1, hakuzitendea haki dakika alizocheza za kipindi cha pili.

Kutokana na kiwango alichonacho kwa sasa, amekuwa akisugulishwa benchi na ilibakia kidogo auzwe AFC Leopard ya nchini Kenya, katika kipindi hiki cha dirisha dogo, lakini ikashindikana na kwa mwendo huu anaokwenda nao, ni wazi msimu huu ukimalizika yeye atakuwa mchezaji wa kwanza kutemwa kama hatabadilika.

Nimekaa nikawa najiuliza nani mchawi wa Mrundi huyu? Je, ni kutokana  na kutojituma mazoezini? Au je…

Kwa habari zaidi usikose kununua nakala yako

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*