googleAds

Nandy Festival hapatoshi Kahama

NA SICSA MACHABA

BAADA ya kufanya vizuri mkoani Tanga, tamasha la Nandy Festival, leo linatarajiwa kuwasha moto wa burudani kwa mashabiki wa Mji wa Kahama ndani ya Uwanja wa Taifa.

Nandy, ameliambia Papaso la Burudani kuwa maandalizi yamekamilika na leo ataongoza wasanii kama Rostam (Roma na Stamina), Marioo na Dogo Janja, kuwapa burudani mashabiki mjini huko kabla ya kesho kuhamia Shinyanga.

“Kiukweli tumejipanga vizuri kuwaburudisha wakazi wa Kahama vile vile tarehe 17, tutakuwa Shinyanga, nitakuwa mimi na wasanii wengine nilioambatana nao, kwahiyo mashabiki zangu tukutane pale kuanzia saa 12 jioni,” alisema Nandy.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*