googleAds

Naiona Singida United inashuka daraja

NA ONESMO KAPINGA

LIGI  Kuu Tanzania Bara, inaendelea kupamba moto, huku Simba wakiendelea kufanya vizuri kuhakikisha wanatetea ubingwa kwa mara nyingine ili waweze kuiwakilisha nchi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba ambayo mwaka juzi ilifanikiwa kufika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, mwaka jana ilitolewa hatua ya awali na timu ya UD Songo ya Msumbiji.

Mabingwa hao wa Tanzania, walitolewa nyumbani kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Msumbulji, timu hizo zilitoka sare ya kutofungana, hivyo UD Songo kusonga mbele kwa faida ya bao la ugenini.

Nikiiangalia Simba ambayo kwa sasa inaongoza Ligi Kuu Bara kwa pointi 47,  baada ya kucheza michezo 18, ikishinda 15, sare mbili na kupoteza mmoja, timu ya Singida United  inapumulia mashine.

Singinda United pamoja na kufanya usajili kipindi cha dirisha dogo lililofungwa Januari 15, mwaka huu, bado inaonekana kuchechemea kutokana na matokeo mabaya.

Timu hiyo hadi sasa imecheza michezo 18 na ndiyo inayoshika mkia kutokana na pointi 10, ikiwa imeshinda mara mbili sare nne na kupoteza michezo 12.

Matokeo hayo ni dalili mbaya kwa Singida United,  kwani ikiendelea na mwenendo huo, itakuwa ni msimu wake wa mwisho wa kushiriki ligi  hiyo.

Mzee wa Kupasua anaiona ileeeā€¦Singida United inashuka daraja taratibu  na hakuna mtu  mwingine atakayelaumiwa zaidi ya viongozi wa klabu hiyo.

Viongozi wa Singida United  wameshindwa kuiwezesha timu yao kucheza soka ya ushindani, licha ya kuboresha kikosi chao kwa kusajili wachezaji wengi waliochoka.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*