Nadal aweka rekodi Frech Open

PARIS, Ufaransa

NYOTA wa tenisi, Rafael Nadal, amelibeba taji la Michuano ya Wazi ya Ufaransa (French Open) kwa kumchapa Dominic Thiem katika mchezo wa fainali na hiyo ni rekodi kwake.

Akimchapa Thiem kwa seti 6-3 5-7 6-1 6-1, Nadal raia wa Hispania, anakuwa mchezaji wa kwanza kulibeba mara 12 taji la michuano hiyo.

Kwa upande mwingine, baada ya mchezo huo wa fainali, Thiem alimpongeza bingwa huyo kutokana na rekodi hiyo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*