MZANI ‘UMEBALANCE’ SPORTPESA SUPER CUP

NA LULU RINGO


Mzani ‘umebalance’ michuano ya Kombe la Sportpesa… ndivyo unavyoweza kusema baada ya Timu ya Singida United kutinga nusu fainali baada Simba SC iliyofuzu hatua hiyo jana.

Timu hizo mbili sasa zitakutana na timu za Kenya zilizofuzu hatua hiyo ambazo ni Gor Mahia na Kakamega Homeboys huku Yanga na JKU (Tanzania) na Kariobangi na AFC (Kenya), zikiwa zimeshaaga mashindano hayo.

Singida United imefuzu hatua hiyo baada ya kuilaza AFC Leopard ya nchini Kenya kwa mikwaju ya penati 4-2 baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika bila timu  hizo kufungana.

Wapigaji wa penati hizo kutoka Singida walikuwa Keny Ally Mwambungu, Miraji Adam, Dany Lyanga, Sumbi Elinyesia na Shafiq Batambuzi, wachezaji wa AFC Leopard walikuwa Kambura, Wkooya na Isuza.

Michuano hiyo Sportpesa itatimua vumbi tena kwa timu zilizotinga nusu fainali kukutana Alhamisi ambapo Simba atachuana na Kakamega Homeboys huku Singida ikikutana na Gor Mahia.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*