Mwigizaji Mkenya mwenye ndoto za kumnasa Denzel Washington

NA BRIGHITER MASAKI

TASNIA ya filamu nchini, inazidi kukua kiasi cha kuwavutia wasanii kutoka nje ya mipaka yetu wakitaka kushirikiana nao ili kwa pamoja sanaa ya uigizaji iendelee kupiga hatua.

BINGWA limekutana na Luwi Hausa, jijini Nairobi, Kenya, mwigizaji nyota wa tamthilia ya Maria inayoruka katika kituo cha runinga cha Citizen Tv na kuzungumza naye kuhusu mambo mengi ya sanaa.

Brian Martin’s Ogana, ndiyo jina lake halisi alilopewa na wazazi wake, baada ya kuzaliwa miaka 32, iliyopita akiwa ni mzaliwa wa kwanza katika familia ya watoto watatu na wadogo zake wawili wa kike na wa kiume.

Anasema ana elimu ya Chuo Kikuu cha Nairobi  na kupata shahada ya uhadisi wa kompyuta na baadaye akasoma kozi fupi ya uandishi wa habari.

“Ni baba mwenye wa watoto watatu, ambapo wasichana wawili na mvulana mmoja nip-o na mtu ambaye si maarufu,” anasema.

Luwi anasema ameokoka na hutumia muda mwingi katika kukaa na familia yake, kusoma vitabu, kuogelea, kusafiri, mitindo, ushairi na upishi.

“Nilianza sanaa tangu nilipokuwa mdogo nikiwa  darasa la pili na baba yangu ndiye alinifanya nipende sanaa kwa kunifanya nimfuatilie Shakespeare katika kusoma na kuigiza vitabu vyake.

 “Ukiachana na suala zima la sanaa, pia nina maduka yangu ya biashara za suti kama unaangalia vizuri kwenye tamthilia ya Maria, suti ambazo ninazivaa kwenye vipindi vyote nimezishona mwenyewe na pia nauza,” anasema Luwi.

Anaongeza kuwa mama yake ndiye aliyemfundisha kushona na hajawahi kushiriki tukio lolote la mitindo bali huwashonea wateja wanaofurahia bidhaa zake.

 “Nimebahatika kutoa ajira kwa vijana wenzangu, nina jumla ya wafanyakazi saba wanaonisaidia, wateja ni wengi hivyo mtu mmoja hauwezi kuwahudumia wote kwa pamoja unahitaji usaidizi. anasema.

 “Pia waigizaji ambao ninawapenda sana ni Denzel Washington, Liam Neeson, Will Smith na Kenya ni Raymond Ofula, Dennis Musyoka na Gilbert Lukalia.

“Ndoto yangu kubwa napenda kufanya kazi na Denzel Washington, Desmond Eliot na Ramsey Nouuh ni wasanii ninao waangalia nawakubali sana,” anasema Luwi.

Kuhusu tasnia ya filamu Bongo,  Luwi anasema:  “Ninapenda nchi ya Tanzania na nimeshawahi kuitembelea mara kadhaa, kuna wanamuziki ninaowapenda kama Ali Kiba, Diamond Platinumz na Lady JayDee na wafuatilia mno.”

Aliongeza kuwa:   “Natamani nikija kwa mara nyingine ningependa sana kufanya kazi na Vicent Kigosi ‘Ray’ kwa jinsi anavyofanya kazi zake na kuzifikisha kwenye jamii ni maisha halisi ya kiwango kingine cha sanaa ya juu.

“Napenda pia muziki wa zamani ya Profesa Jay, ingawa sijui kama bado anaimba, baada ya kuwa Mbunge pia Gabo Zigamba na Yusuf Mlela ni wasanii ninaowapenda.”

Luwi anasema wasanii kama Mimi Mars, Vanessa Mdee na Elizabeth Michael ‘Lulu’ ni watu wake wa karibu na wamekuwa washauri wazuri kwenye sanaa yake.

“Nilianza rasmi uigizaji mwaka 2005. Uzoefu umenifundisha kutojihusisha na mahusiano mahali ninapofanyia kazi sababu mambo huharibika lakini huwezi kujua ya Mungu ni mengi na chochote kinaweza kutokea.
 “Nina kawaida kutoa msaada kwa jamii inayonizunguka hasa watu wenye uhitaji. Nina mpango wa hutoa pesa za usafiri kwa wanafunzi wa shule za sekondari, hasa walio katika hali ngumu ya kimaisha.”

 
 
                                          
 
 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*