googleAds

Mwantika fasta arudishwa Misri

NA ZAINAB IDDY

BEKI wa Azam FC, David Mwantika, amerudishwa tena nchini Misri kujiunga na kikosi cha Taifa Stars kitakachoshiriki michuano ya AFCON inayoanza kesho.

Awali Mwantika alikuwa amtemwa katika kikosi cha mwisho cha wachezaji 23 lakini kocha mkuu wa Stars, Emmanuel Amunike, amelazimika kumrudisha kundini kuziba pengo la Aggrey Morris aliyepata majeraha katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Misri.

Akizungumza na BINGWA jana, Meneja wa Taifa Stars, Danny Msangi, alisema jeraha la goti alilolipata Morris wakati wa mchezo ho wa kirafiki ambapo Stars ilifungwa 1-0, limemfanya kukosa michuano hiyo mikubwa barani Afrika. 

“Kiafya Morris hayupo sawa na kwa mujibu wa daktari, hataweza kucheza, hivyo basi kocha amependekeza nafasi yake ichukuliwe na Mwantika ambaye ataingia Misri leo (jana) na kuungana na wenzake,” alisema Msangi. 

Taifa Stars wataanza mchezo wao wa kwanza Kundi C Jumapili dhidi ya Senegal ambayo itamkosa Saido Mane anayetumikia adhabu kabla ya kuwavaa Harambee Stars ya Kenya na kumaliza hatua ya makundi dhidi ya Algeria. 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*