googleAds

Mwambusi afurahia kiporo Yanga

NA  ZAINAB IDDY

BENCHI la ufundi la Mbeya City, limesema kuwa  kitendo cha kusogezwa mbele kwa mechi yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga kimewapa nafasi ya kuendelea kukiandaa vyema kikosi chao.

 Mchezo wa Mbeya City na Yanga  ulikuwa uchezwe Septemba 18, mwaka huu,  Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, lakini  umehairishwa ili kuwapa nafasi Wanajangwani kufanya maandalizi yao kuelekea mechi ya marudiano ya  Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zesco United ya Zambia.

Akizungumza na BINGWA jana  Kocha wa timu hiyo, Juma Mwambusi alisema bado yupo katika kukijenga kikosi chake chenye wachezaji wengi wageni,  hivyo kusongezwa mbele kwa mechi yao ni faraja kwao.

“Nilisema tangu awali nahitaji muda zaidi kuijenga timu ya ushindani kwa sababu kuna wachezaji wengi wapya na wageni kwenye ligi, hivyo TFF kusogeza mbele mechi yetu ni jambo zuri kwangu.

“Ninahakika hadi tutakapocheza Ruvu Shooting kwa mechi itakayofuata  nitakuwa tayari nimepata muunganiko mzuri wa timu mbao ninauhitaji, ”alisema.

Next Article

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*