googleAds

Mwalala atoa ushauri Yanga

MWAMVITA MTANDA

KOCHA wa timu ya Bandari ya Kenya, Ben Mwalala, amesema klabu yake ya zamani ya Yanga, inatakiwa kusajili mshambuliaji mwenye uwezo zaidi  kama ina mipango ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao.

Akizungumza na BINGWA jana  kutoka Kenya, Mwalala alisema ameangalia  mkanda wa video  wa mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Township Rollers uliochezwa wiki iliyopita Uwanja wa Taifa,Dar es Salaam , hajaona mshambuliaji msumbufu kwa Wanajangwani hao.

Mwalala alisema katika eneo la mabeki na viungo hajaona tatizo, kwani walicheza vizuri, licha ya kutoka sare ya bao 1-1.

“Hata kama kuna mfumo mpya wa soka, lakini timu lazima ipate namba kamili ya mshambuliaji, kwa Yanga bado kuna mapungufu, ni timu ambayo nilishacheza natambua  wachezaji wanaostahili kuwepo.

“Nikisema hivyo sina maana kuwa kikosi ni kibovu ila  kinatakiwa kiwe na ari ya mapambano, washambuliaji makini hata wawili wazuri ili wawezi kutimiza malengo yao,” alisema Mwalala.

Mwalala alisema licha ya kuwapo kwa  mshambuliaji wanayemtumania David  Molinga kuwa anauwezo lakini  anahitaji muda wa kutosha ili aweze kufanya vizuri.

“Nimeangalia mkanda wa video ya Molinga akiwa FC Lupopo, ni mziri lakini kwa mazingira mapya anahitaji muda wa kutosha kujifua,” alisema Mwalala.

Akizungumzia makipa,  Mwalala alisema anamfahamu Farouk Shikalo, aliyesajiliwa na Yanga kutoka Bandari ya Kenya ni kipa mwenye uwezo mkubwa  hivyo walifanya chaguo zuri kumsajili na atawasaidia.

Mwalala alisema kipa mwingine ambaye anaweza kuwasaidia Yanga ni kinda Ramadhani Kabwili  naye ana uwezo wa kudaka.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*