googleAds

Muivory coast wa Azam azidi kunoga

JESSCA NANGAWE NA TIMA SIKILO

UONGOZI wa klabu ya Azam FC umemwongezea mkataba wa miaka miwili mshambuliaji wake raia wa Ivory Coast, Richard Djodi.

Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Abdulkarim Amin ‘Popat’, alisema wamefikia uamuzi huo kutokana na uwezo wake uwanjani.

“Ameonyesha uwezo mkubwa na sisi tumevutiwa naye kwa kipindi kifupi tulichokua naye na kuamua kumwongezea mkataba, sasa tutaendeela kuwa naye kwa kipindi chote hiki,” alisema Popat.

Straika huyo alisajiliwa msimu huu na Azam FC kwa mkataba wa mwaka mmoja, na sasa ameogezewa mkataba mwingine ambao utamalizika mwaka 2022.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*