Mtibwa kutumia Uwanja wa Azam

NA TIMA SIKILO

KLABU ya Mtibwa Sugar, imepanga kutumia uwanja wa nyasi bandia wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika,  inayoanza mwezi huu.

Akizungumza na BINGWA jana, Mkurugenzi wa klabu  hiyo, Jamal Bayser, alisema wamepanga kutumia uwanja wa Azam kutokana na ule wa Jamhuri Morogoro, kutokidhi viwango vya kimataifa.

“Ni kweli tutatumia Uwanja wa Chamazi kama uwanja wa nyumbani katika michuano ya kimataifa, hii inatokana na ule wa Jamhuri kutokidhi kiwango vya kimataifa, hivyo tukaona tuchague uwanja huo kutokana na ushirikiano mzuri tulionao na Azam,” alisema.

Akizungumzia maandalizi ya timu hiyo, Bayser alisema kikosi chao kimeingia kambini kujiandaa na michuano hiyo.

Mtibwa Sugar wataanza kucheza na Northern Dynamo ya Shelisheli, katika mchezo wa awali utakaochezwa kati ya Novemba 27-28, mwaka huu na kurudiana Desemba 5, jijini Victoria.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*