MTIBWA KUSAJILI WANNE WAPYA

NA SAADA SALIM


MTIBWA Sugar wanatarajiwa kusajili wachezaji wanne wapya katika usajili mdogo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, unaoendelea hivi sasa.

Akizungumza na BINGWA, Mkurugenzi wa klabu hiyo, Jamal Bayser, amesema wamepokea ripoti ya kocha wao, Salum Mayanga na amependekeza wachezaji wanne waongezwe katika idara ya kiungo na ushambuliaji.

Bayser alisema watafanyia kazi ripoti hiyo ili kutimiza matakwa ya benchi la ufundi.

“Ni kweli ripoti imetufikia, tumeiangalia vizuri na tutafanya kile ambacho kocha wetu amekipendekeza, ambapo anataka tumuongezee wachezaji wanne, hilo kwetu halina shida, kwani tunachohitaji ni kuiona Mtibwa Sugar kupata ushindi.

Amependekeza aongezewe nguvu katika idara ya kiungo na ushambuliaji,  anataka mzunguko wa pili afanye makubwa, kitu ambacho hata sisi tunakitamani sana,” alisema Bayser.

Katika ripoti wa Mayanga, amependekeza kumrejesha kiungo wa timu hiyo, Awadh Juma, ambaye hana namba kwenye kikosi cha kocha wa Simba, Joseph Omog.

Wachezaji wa timu wameingia kambini kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu utakaoanza Desemba 27, mwaka huu.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*