googleAds

MSUVA ARUDI KIVINGINE YANGA

NA ZAINAB IDDY


WAKATI Yanga wakitarajiwa kuanza mazoezi kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, winga wa timu hiyo, Simon Msuva, amesema atarejea dimbani kivingine.

Yanga wataanza mazoezi leo kwenye Uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini, jijini Dar es Salaam chini ya kocha mkuu mpya, Mzambia George Lwandamina, baada ya Hans van der Pluijm,  kubadilishiwa majukumu na kuwa mkurugenzi wa timu hiyo.

Akizungumza na BINGWA jana, Msuva alisema kipindi cha mapumziko hakuweza kulala, kwani alikuwa anaendelea kujifua kivyake ili kulinda kipaji chake.

Msuva alisema akiwa mapumzikoni ajipangia programu ya mazoezi ili kuhakikisha anajiweka fiti zaidi kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi hiyo.

“Kama nilivyowahi kusema msimu huu wa ligi kwangu nataka uwe tofauti kwa kuhakikisha naisaidia timu yangu kwa asilimia 100 na kufunga mabao,” alisema Msuva.

Alisema hakuweza kukatisha mazoezi akiwa mapumzikoni, kwani waliendelea kufanya mazoezi ya viungo ‘gym’  kwa faida ya mwili wake.

Akimzungumzia Lwandamina, alisema anaamini watafanya naye kazi vizuri kama ilivyokuwa kwa Pluijm.

“Sina shaka na mabadiliko ya benchi la ufundi, nina uhakika tutafanya kazi vizuri na kocha mpya, Pluijm anayetujua bado yupo hivyo wana-Yanga watarajie kuona soka la ushindani kutoka kwetu.”


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*