googleAds

MSUVA APATA KIGUGUMIZI UFUNGAJI BORA

NA SALMA MPELI,

WINGA wa Yanga, Simon Msuva, ameshindwa kuzungumzia hatima yake katika vita ya kuwania tuzo ya ufungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Hatua hiyo ya winga huyo imekuja baada ya mwishoni mwa wiki  kuumia  akiwa katika harakati za kuifungia Yanga bao wakati wa mechi dhidi ya  Mbeya City iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, mwishoni mwa wiki ambapo Jangwani ilishinda mabao 2-1.

Msuva aliumia baada ya kugongana na mchezaji wa Lyon, Thumba Lui na kusababisha kupasuka juu ya jicho na kushonwa nyuzi sita.

Msuva ambaye anaongoza katika orodha ya wafungaji wa ligi hiyo akiwa amepachika wavuni mabao 14, jana alikataa kuzungumzia vita ya ufungaji kwa madai kwamba hali yake kiafya si shwari.

“Siwezi kuongelea suala hilo kwa sasa kwanza hali yangu bado na sitaweza kucheza mechi ya kesho, lakini ligi bado haijamalizika hadi kwenye mchezo wa mwisho ndiyo tutajua nani ataibuka mfungaji bora,” alisema Msuva.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*