Mshindi Singeli Michano Dodoma ahamia Dar

NA JEREMIA ERNEST

MSHINDI wa shindano  la Singeli Michano Dodoma mwaka jana, Steven Johan ‘MC Stizo’, ameweka wazi kuwa ameamua kuhamia Dar es Salaam ili kupambana kutoka kimuziki.

Akizungumza na Papaso la Burudani, Mc Stizo alisema shindano hilo linaloendeshwa na kituo cha redio E Fm, lilimfungulia milango kwani mpaka sasa ameshafanya kolabo tatu na wasanii wakubwa wa muziki huo.

“Nimeona Dodoma hakuna ushindani hasa katika muziki wa singeli, nimekuja Dar es Salaam ili nipambane na niweze kutoka, muziki unahitaji upinzani na sasa nipo tayari kupambana,” alisema Stizo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*