Mrithi wa Mwambusi kufumua kikosi Mbeya City
NA ZAINAB IDDY
KAIMU Kocha Mkuu wa timu ya Mbeya City, Mohamed Kijuso, amesema ataisuka upya safu ya ushambuliaji na ulinzi, dirisha dogo la usajili litakapofunguliwa Desemba 16, mwaka huu.
Kijuso aliyekuwa kocha msaidizi, baada ya Juma Mwambusi kujiuzulu, amekabidhiwa kusimamia kikosi hicho.
Akizungumza na BINGWA jana, kutoka mkoani Mbeya, Kijuso, alisema safu ushambuliaji imekuwa butu tangu waliponza Ligi Kuu Tanzania Bara, msimu huu, hivyo ni lazima afumue kikosi hicho.
“Ukiangali katika mechi 12 tulizocheza tumeshinda mabao nane tu, ni idadi ndogo mno, pia sehemu ya ulinzi inakosa umakini kutokana na kuruhusu mabao mengi kuliko timu nyingine za ligi.
“Kwa hali hii lazima yafanyike mabadiliko kipindi cha dirisha dogo ili kuinusuru timu katika hatari ya kushuka daraja msimu huu.”
Leave a Reply