Mpira wa meza Z’bar walia na vifaa, udhamini

NA VICTORIA GODFREY

CHAMA cha Mpira wa Meza Zanzibar (ZTTA), kinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vifaa vya mchezo huo hivyo kukwamisha mipango yao visiwani humo.

Akizungumza na BINGWA jana kutoka Zanzibar, Mwenyekiti wa ZTTA, Latifa Daud Jussa, alisema wachezaji wao wengi wanakwamishwa na vifaa vya mazoezi ya mchezo huo hivyo kushindwa kushiriki mashindano mbalimbali.

Alisema  kuwa  changamoto nyingine  ni ukosefu wa udhamini ambao umekuwa ukikwamisha uandaaji wa mashindano mbalimbali yawe katika viwango ambapo hadi wasubiri kupata ruzuku serikalini.

“Kwa hizi changamoto  ndio zinazotukabili katika mchezo huu kutokana na tunashindwa kufikia malengo yetu, kama tukifanikiwa kupata, tunaweza kusonga mbele zaidi na kupata wachezaji watakaopata nafasi timu ya taifa na kuitangaza nchi na Zanzibar pia,” alisema Latifa.

Latifa alisema kuwa tayari hatua mbalimbali zimechukuliwa pamoja na kuzungumza na Serikali na imewaahidi kuwatatulia changamoto ya vifaa kwa kutoa baadhi ya vifaa, zikiwamo meza.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa hatua nyingine ya ufadhili ni kutafuta kampuni, taasisi na kufanya mazungumzo nao ili waweze kutoa udhamini ili kuweza kutekeleza mipango ya chama katika kuendeleza mchezo huo.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*