Mourinho awapiga ‘stop’ Wachina

LONDON, England

KOCHA wa zamani wa Manchester United, Jose Mourinho, ameripotiwa kugoma kupokea kitita cha pauni milioni 88 (sh bil.252) ili kuinoa Guangzhou Evergrande ya Ligi Kuu China.

Mourinho hakujihusisha na masuala ya soka tangu alipofungashiwa virago na Manchester United mwaka jana.

Kituo cha televisheni cha Sky Sports, kimeripoti kuwa endapo Mourinho atakubali dili hilo, atakuwa miongoni mwa makocha wanaolipwa mkwanja mrefu duniani.

Imeripotiwa kuwa Mouriho alikutana na bilionea wa klabu hiyo, kuzungumza kuhusu dili hilo, kabla ya kupiga chini na kugoma kusaini mkataba mnono wenye ‘pesa ndefu’ (fedha nyingi).

Alipoulizwa kuhusu taarifa hiyo, Mourinho alidai mipango yake ni kufundisha timu ya taifa na si katika ngazi ya klabu.

“Kwa miaka kadhaa, nimekuwa na tamaa ya kujaribu katika ngazi ya Kimataifa, kwasasa nafikiria Kombe la Dunia na michuano mikubwa,” alisema Mourinho.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*