MOURINHO AMTABIRIA MABAYA MATIC

Moscow, Urusi

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho, amemuombea Nemanja Matic na timu yake ya taifa ya Serbia, kuondoshwa mapema katika fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu.

Kauli hiyo ilikuja kutokana na nyota huyo kutopata muda mwingi wa  kupumzika tangu kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu ya England hapo Mei 13.

“Ni ngumu sana, sitaki kufikiriwa vibaya lakini nawahitaji wachezaji wangu warudi mapema kwa ajili mapumziko ya kujiandaa na msimu ujao,” alisema Mourinho kupitia televisheni ya RT America.

“Nataka Matic apate mapumziko, hivyo nawatabiria Uswis kumaliza nafasi ya pili katika kundi lao. Niombe radhi kwa mchezaji wangu ila ukweli ndiyo huo.”


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*