Mourinho amgeukia Mahrezi.

MANCHESTER, England

USIKU wa leo dirisha la usajili litafungwa, lakini huenda Riyad Mahrez akawa Old Trafford kabla ya muda huo.

Jina lake liko kwenye meza ya mabosi wa Manchester United na imeelezwa ni kocha Jose Mourinho ndiye anayemtaka kwa udi na uvumba.

Winga huyo wa Leicester ameshauomba uongozi wa klabu yake hiyo kumwacha na Mourinho anamtaka kwa kuwa haoni uwezekano wa kumchukua Ivan Perisic wa Inter Milan.

Katika hatua nyingine, ni kama Mourinho amepuuzia taarifa za hivi karibuni zilizodai Mwafrika huyo raia wa Algeria atabaki Leicester kwa msimu mmoja zaidi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*