MOURINHO AJISHEBEDUA KUFUTIWA MASHTAKA FA

LONDON, England


 

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho, amejishebedua akisema kuwa alikuwa anauhakika kwa asilimia 100 kwamba hakutumia lugha ya matusi kama alivyofunguliwa mashtaka na Chama cha Soka England (FA).

Chama cha Soka England (FA), kilimfungulia mashtaka, Mourinho ya kutumia lugha chafu wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ambao Manchester United waliondoka na ushindi wa mabao 3-2  dhidi ya Newcastle United, lakini yakafutwa juzi.

Akizungumza jana kwenye mkutano wake na waandishi wa habari wa kuzungumzia mechi yao ya leo dhidi ya Bournemouth, Mourinho alisema kwamba hakumdhalilisha wala kumshambulia mtu ama kuonesha utovu wa nidhamu mbele ya kamera.

“Niliiomba klabu na wakili wakate rufaa kwa sababu nilikuwa na uhakika kwa asilimia 100 sikuwa na kosa katika mashtaka haya,” alisema kocha huyo.

“Lakini siwezi kufahamu kilichojitokeza ila nilikubali na kuheshimu walichonishitakia na ikanibidi nisubiri ili nione kitakachojitokeza,” aliongeza Mourinho.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*