googleAds

MOLINGA AMKABA KOO MAKAMBO

NA MAREGES NYAMAKA

WAKATI baadhi ya mashabiki wa timu ya wananchi, Yanga wakiendelea kumkumbuka straika wao wa zamani, Heritier Makambo, wakidai ni bora angebaki kikosini hapo kutokana na makali yake, lakini bado kitakwimu hana tofauti na straika wa sasa David Molinga.

Hatua hiyo inakuja baada ya Molinga aliyecheza mechi zote tatu za Ligi Kuu Bara kufunga mabao mawili. Molinga alishindwa kutupia katika mechi ya kwanza ya ligi dhidi ya Ruvu Shooting lakini akaingia kambani mara mbili Yanga ilipocheza na Polisi Tanzania. Katika mechi ya mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Coastal Union, straika huyo hakufurukuta.

Takwimu zinaonyesha, idadi kama hiyo ya mabao ya Molinga aliyofunga katika mechi tatu ni sawa na ile ya Makambo.

Straika huyo wa zamani wa Yanga ambaye anakipiga Horoya ya Guinea, alianza kufungua akaunti ya mabao katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Mtibwa Sugar likiwa ni bao la kuongoza akimalizi kwa kichwa krosi ya Gadiel Micheal, huku bao la pili katika mchezo huo likifungwa na Kelvin Yondan kwa mkwaju wa penalti.

Mchezo uliofuata Septemba 16 mwaka jana, licha ya Yanga kuibuka na ushinda wa mabo 4-3 dhidi ya Stand United, Mcongo huyo aliondoka patupu, lakini siku nne baadaye alirejesha makali yake akifunga bao pekee na la ushindi dhidi ya Coastal Union.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Makambo alifunga bao hilo dakika ya 11 akimaliazi kwa guu la kushoto mpira ulichongwa na Ibrahim Ajib.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*