googleAds

Mo Rashid afurahia kwenda JKT Tanzania

NA MWANDISHI WETU

MSHAMBULIAJI wa Simba, Mohamed Rashid ‘Mo Rashid’,  amesema anaamini kufanya kazi tena na kocha wake, Abdallah Mohamed ‘Bares’  kutarejesha makali  yake ya kucheka na nyavu kama ilivyokuwa misimu miwili iliyoipita.

Rashid anatarajia kujiunga kwa mkopo JKT Tanzania inayonolewa na Bares, baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo KMC, aliyoisaidia msimu uliopita kumaliza nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara huku akipachika mabao 10.

Mshambuliaji huyo alijiunga na Simba kwa mkataba wa miaka mitatu msimu uliopita, akitokea Tanzania Prisons, lakini alijikuta akikosa nafasi ya kucheza mara kwa mara kutokana na kuwapo kwa washambuliaji wengine bora katika kikosi cha Wekundu hao, akiwemo Johm Bocco, Emmanuel Okwi na Meddie Kagere.


Akizungumza na BINGWA jana, Rashid alisema, licha ya kutakiwa na timu za Kagera Sugar na Prisons, lakini ameamua kumfuata kocha wake huyo ambaye anaamini atamsadia kurudisha makali yake.

“Mimi ni mchezaji na nipo tayari kucheza timu yeyote ile, kikubwa ni makubaliano na viongozi wangu wa Simba, lakini nina nafasi ya kufanya uamuzi binafsi juu timu nitakayojiunga nayo, na katika hilo nitaipa kipaumbele ile ambayo itanipa nafasi ya kucheza mara kwa mara.

“Nafikiri JKT Tanzania ni sehemu nzuri zaidi kwangu kwa kuwa yupo kocha ambaye ananifahamu vizuri, tumefanya kazi pamoja na anajua utendaji wangu,
nina imani ya kufanya vizuri tena kama ilivyokuwa misimu miwili iliyopita nikiwa chini yake tena,” alisema 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*