MKWASA AUNDIWA ZENGWE

NA MWANDISHI WETU

KATIBU Mkuu wa Klabu ya Yanga, Charles Mkwasa ameundiwa zengwe la kung’olewa kwenye nafasi yake na watu waliopo ndani ya klabu hiyo wanaotaka kupiga fedha watakazochuka wakitinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Timu ya Yanga baada ya kufanikiwa kushinda mechi ya awali ya mtoano dhidi ya Walayta Dicha kwa mabao 2-0, imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele na  kuanza kuchukua fedha zinazotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Endapo Yanga itaingia hatua ya makundi inatarajiwa kupata kiasi cha dola za Kimarekani Dola 150,000 (Sh 330 Milioni).

Inadaiwa kundi hilo linaongozwa na mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Mashindano, ambaye anataka kiongozi huyo aondoke ili nafasi hiyo ichukuliwe na mtu mwingine.

BINGWA lilimtafuta Mkwasa na kusema kuwa hana taarifa zozote juu ya suala hilo, ila kama kuna watu wanahitaji nafasi yake yupo tayari kuwapisha bila kutumia nguvu.

“Sijasikia kitu kama hicho, mimi ninachowaomba wasitumie nguvu kubwa kufanya hilo jambo, kama kuna mtu wao wanataka kumuweka aje tu nitampisha hakuna shida,” alisema Mkwasa.

 


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

*
*